AFRIKA
1 dk kusoma
Shirika la ndege la Kenya Airways laimarisha safari zake za Ulaya
Shirika la ndege la Kenya Airways limeongeza safari zake za Ulaya kwa kuanza kutuwa katika uwanja wa ndege wa London Gatwick Julai 2025
Shirika la ndege la Kenya Airways laimarisha safari zake za Ulaya
Shirika la ndege la Kenya Airways. / Reuters
3 Julai 2025

Shirika la ndege la Kenya Airways (KQ) limezindua safari za ndege za moja kwa moja kutoka Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, Nairobi hadi Uwanja wa Gatwick, London Julai 2, 2025.

Shirika hilo litakuwa linafanya safari tatu kwa wiki kuelekea Gatwick— siku za Jumatano, Ijumaa, na Jumapili— safari hizi za ndege zitaongeza idadi ya zile zinazoelekea Uwanja wa ndege wa London Heathrow, na kufanya idadi ya safari za kuelekea London kuwa 10 kwa wiki.

Pamoja na hayo shirika hilo linasema ni miongoni mwa mikakati ya kuongeza safari zaidi na kuwapa abiria fursa ya kutuwa katika uwanja wa pili wa ndege nchini Uingereza.

Afisa Mkuu Mtendaji wa Kenya Airways Allan Kilavuka alieleza umuhimu wa safari hizi kwa biashara, utalii, na kuimarisha ushirikiano na watu wa diaspora, kuashiria uwezekano wa kupanua zaidi soko la Uingereza:

“Tumefurahia sana kuongezeka kwa Uwanja wa Ndege wa Gatwick katika mtandao wetu kumaanisha kuwa wateja wa KQ wanaweza kuchagua wapi wanapotaka kutuwa wakati wa safari zao za ndani na nje ya Uingereza wakiangazia ratiba inayowafaa.” Aliongeza Kilavuka.

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us