Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Leo XIV ameonyesha hofu ya kuzorota kwa hali ya usalama kati ya Iran na Israel.
Iran imeirushia Israel makombora ya kulipiza kufuatia mashambulizi ya Israel, hivyo kuzua hofu kubwa ya kuzuka kwa vita katia eneo hilo la mashariki ya kati.
Papa Leo ameomba nchi hizo mbili kuwajibika na kuwa na nia njema.
“Ahadi ya kujenga ulimwengu salama, usio na vitisho vya nyuklia, inapaswa kutekelezwa kwa njia ya kuheshimiana na mazungumzo ya dhati, ili kujenga amani ya kudumu inayosimikwa katika haki, udugu na manufaa ya wote. Hakuna mtu anayepaswa kutishia uwepo wa mwingine,” Papa Leo XIV amesema katika mtandao wa X.
“Ni wajibu wa nchi zote kuunga mkono suala la amani, kuanzisha njia za upatanishi na kuendeleza suluhu inayohakikisha usalama na utu kwa wote!”