Koitalel Arap Samoei aendeleza alipoachia baba yake
Koitalel Arap Samoei aendeleza alipoachia baba yake
Kwa kipindi cha zaidi 10, aliendesha mapambano dhidi ya vikosi vya Waingereza, hususani uwepo wa reli ya Uganda.
2 Juni 2025

Baada ya kuuwawa kwa Kimnyole Arap Turukat, wengi waliamini kuwa kazi ya utabiri ilikuwa imekwisha.

Hawakujua kuwa, ataibuka mtoto wake, aitwae Koitalel Arap Samoei, ambaye atakuja kubeba maono ya baba yake mzazi.

Akiwa amezaliwa mwaka 1860 katika eneo la Samitu, Aldai, Koitalel alikuwa zaidi ya kiongozi.

Hakuwa amerithi cheo cha baba yake tu, bali maono na maonyo yake.

Yeye pia, alitabiri ujio wa “nyoka mweusi”, yaani reli ya ‘wazungu’.

Baada ya kufikisha umri wa 25, Koitalel akatawazwa kuwa Orkoiyot—kiongozi wa kiroho na shujaa wa vita.

Kwa kipindi cha zaidi 10, aliendesha mapambano dhidi ya vikosi vya Waingereza, hususani uwepo wa reli ya Uganda.

Hata hivyo, hakujua kuwa alikuwa anasubiri kusalitiwa.

Oktoba 19, 1905, afisa muingereza, aliyejulikana kama Richard Meinertzhagen alimwita kwa ajili ya mazungumzo ya kutafuta amani.

Hata hivyo, Koitalel aliuwawa wakati wa kikao hicho, huku Waingereza wakiutenganisha mwili wake, na kuchukua fuvu lake na kwenda kulihifadhi jijini London.

Ingawa kifo chake kiliashiria kumalizika kwa vita vya Nandi, bado kiliongeza vuguvugu la upinzani.

Miaka michache baadaye, mtoto wake, Barsirian Arap Manyei, akawa mfungwa wa kisiasa, akiendeleza urithi kutoka kwa babu yake.

Kufikia leo, Koitalel anaheshimika kama shujaa wa taifa.

Katika eneo la Nandi, makumbusho maalumu imejengwa kwa heshima yake.

CHANZO:TRT Afrika Swahili
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us