AFRIKA
1 dk kusoma
Tanzania kujenga kituo kikubwa cha upandikizaji wa figo Dodoma
Tanzania inatarajiwa kujenga kituo kikubwa cha upandikizaji wa figo katika hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.
Tanzania kujenga kituo kikubwa cha upandikizaji wa figo Dodoma
Hospitali ya Benjamin Mkapa, mjini Dodoma. /BMH
28 Mei 2025

Kituo hicho kinajengwa kwa ushirikiano wa serikali ya Tanzania na shirika la madaktari wa Japan la Tokushukai.

Mradi huo utakapokamilika itakuwa kituo kikubwa zaidi cha upandikizaji wa figo kusini mwa Jangwa la Sahara, ikiwa ni hatua kubwa katika masuala ya huduma za afya na kutoa mafunzo.

Siku ya Jumatatu serikali ya Tanzania ilitia saini makubaliano nchini Japan na shirika la Tokushukai, ambalo kwa muda mrefu limekuwa likiunga mkono juhudi za kuimarisha utoaji wa huduma za afya.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa wakati wa mkutano wa jukwaa la biashara, uwekezaji na utalii la Tanzania na Japan mjini Osaka.

Kituo hicho kitajengwa katika hospitali ya Benjamin Mkapa mjini Dodoma kwa ushirikiano wa shirika la madaktari wa Japan Tokushukai na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). Mradi huo utagharimu zaidi ya dola milioni 10.

Pamoja na kutoa huduma za matibabu, kituo hicho kitatoa mafunzo maalum ya upandikizaji wa figo na kufanya utafiti kwa lengo la kupunguza maradhi yanayotokana na matatizo ya figo.

Mafunzo yatatolewa kwa ushirikiano wa Hospitali ya Benjamin Mkapa na Chuo Kikuu cha Dodoma.

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us