AFRIKA
2 dk kusoma
Rais wa Afrika Kusini asema wananchi wote nchini mwake wana haki sawa
Rais huyo amesema serikali imeanzisha sheria katika maeneo kama vile umiliki wa ardhi, usawa wa ajira na uwezeshaji wa kiuchumi kwa ajili ya kuhakikisha kila mtu anapata haki sawa.
Rais wa Afrika Kusini asema wananchi wote nchini mwake wana haki sawa
Rais Cyril Ramaphosa amesema serikali yake imeanzisha sheria katika maeneo kama vile umiliki wa ardhi, usawa wa ajira na uwezeshaji wa kiuchumi/ Picha: Rais Cyril Ramaphosa / Public domain
28 Mei 2025

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ameongea kuhusu changamoto ambayo inakumba nchi yake kwa sasa, ile ya Marekani kudai kuwa raia wa nchi yake ambao ni wazungu maarufu ‘Afrikaner’ wanateswa.

Tayari Marekani imetoa hifadhi kwa Waafrikaner zaidi ya hamsini na wengine wanatarajiwa kufuata.

“Kila Mwafrika Kusini kwa tafsiri yake ni Mwafrika,” Rais Ramaphosa aliongea bungeni.

“Sisi sote ni wa bara la Afrika kwa usawa, kama vile sote tuko sawa wa Afrika Kusini. Na tunayo madai sawa kwa nchi hii,” Rais huyo ameongezea.

Rais huyo amesema serikali imeanzisha sheria katika maeneo kama vile umiliki wa ardhi, usawa wa ajira na uwezeshaji wa kiuchumi kwa ajili ya kuhakikisha kila mtu anapata haki sawa.

Amesema suala la rangi nchini humo litaendelea kuwa changamoto.

“Katika sensa na ripoti nyengine za takwimu, takwimu za Afrika Kusini hutumia vipengele kama Mwafrika Mweusi, Mrangi, Mhindi/Mwaasia na Mzungu. Utumiaji wa maneno inategemea rangi siku zote na itakuwa mgumu kwa nchi yetu na ni lazima kukubali tunapojitahidi kuweka nyuma dhuluma za rangi za zamani,” Rais Ramaphosa alisema.

Hotuba yake inakuja baada ya ziara yake rasmi ya hivi karibuni nchini Marekani alipokutana na Rais Donald Trump.

“Ziara yetu ilikuja wakati uhusiano kati ya Marekani na Afrika Kusini umekuwa chini ya matatizo yanayoongezeka, hasa kutokana na taarifa potofu zinazorushwa na makundi ya pembezoni katika nchi zetu mbili, ikiwa ni pamoja na simulizi ya uongo kuhusu kile kinachoitwa mauaji ya halaiki na kampeni iliyoratibiwa ya unyanyasaji dhidi ya wakulima wa kizungu,” Rais alisema.

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us