Mahakama ya Afrika Kusini leo Alhamisi imemfunga mwanamke mmoja maisha kwa kumteka na kumuuza binti yake mwenye umri wa miaka sita, katika kesi ambayo imetikisa taifa.
Racquel Smith na wenzake wawili walioshtakiwa pamoa, wamehukumiwa kifungo cha maisha kwa usafirishaji haramu wa binadamu na utekaji nyara wa takriban miaka kumi, kwa mujibu wa Nathan Erasmus.
Mahakama ya Afrika Kusini ilimpata na hatia Smith kwa kumsafirisha kinyume cha sheria binti yake mwenye umri wa miaka sita ambae alipotea kwa zaidi ya mwaka, kesi ambayo imetikisa taifa.
Kesi hiyo iliyosikizwa kwa miezi miwili imesikiliza ushahidi kutoka kwa mashahidi kadhaa ambao Racquel “Kelly” Smith aliwaambia kwamba alimuuza binti yake Joshlin mwezi Februari, 2024, pamoja na madai kwamba alilipwa kiasi cha fedha rand 20,000 sawa na dola 1,085.
Hakimu Nathan Erasmus amesema ushahidi wa mashahidi wa serikali 35 umemfanya abaini kwamba, Smith, 35, na wenzake wawili walioshtakiwa pamoja, mpenzi wake na rafiki, walikuwa na makosa ya biashara haramu ya ushafirishaji wa binadamu na utekaji.
“Tayari nimeona kupitia ushahidi uliowasilishwa kwangu, Joshlin aliuzwa,” amesema.
Ushahidi umeonyesha kumekuwa na malipo, au angalau ahadi ya malipo,” amesema, na kumtuhumu Smith kumuuza binti yake kama bidhaa, aliyekuwa na umri wa miaka sita wakati akipotea.
Hukumu hiyo imetolewa katika ukumbi wa kijamii katika mji mdogo wa wavuvi wa Saldanha Bay, takriban kilomita 135 kaskazini mwa Cape Town, ambapo kesi hiyo iliibua hasira.