AFRIKA
2 dk kusoma
Mwanafasihi maarufu Afrika Mashariki Ngugi Wa Thiong’o afariki dunia
Kulingana Wanjikũ wa Ngũgĩ, ambaye ni binti wa mwanafasihi huyo mahiri barani Afrika, amefariki dunia asubuhi ya Mei 28, 2025, akiwa na umri wa miaka 87.
Mwanafasihi maarufu Afrika Mashariki Ngugi Wa Thiong’o afariki dunia
Ngũgĩ wa Thiong’o afariki dunia
28 Mei 2025

Mwandishi maarufu wa kazi za kifasihi Afrika Mashariki, Ngũgĩ wa Thiong’o amefariki dunia.

Kulingana Wanjikũ wa Ngũgĩ, ambaye ni binti wa mwanafasihi huyo mahiri barani Afrika, amefariki dunia asubuhi ya Mei 28, 2025, akiwa na umri wa miaka 87.

Kabla ya umauti wake, Ngũgĩ wa Thiong’o alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya figo kwa muda mrefu, hali iliyomfanya apate shida ya kutembea.

Pia, alikuwa akipata matibabu ya kusafisha figo zake, huku akigundulika kuwa na maradhi ya saratani ya tezi dume, toka mwaka 1995.

“Tunasikitika kutangaza kifo cha baba yetu, Ngũgĩ wa Thiong’o, kilichotokea asubuhi ya Mei 28, 2025. Aliishi maisha makamilifu, akipigana vita vilivyo vizuri. Kama alivyotaka mwenyewe, tufurahie maisha yake na kazi zake. Rîa ratha na rîa thŭa. Tŭrî aira,” aliandika Wanjiku wa Ngũgĩ katika mtandao wake wa kijamii.

Akiwa amezaliwa Januari 5, 1938, Ngũgĩ, alizaliwa kwa jina la James Ngugi kabla ya kubadilisha jina lake baadaye.

Anajulikana kwa uandishi wa kazi za kifasihi kwa kutumia lugha ya Gikuyu na Kiingereza, pamoja na jitihada zake za kukuza lugha za kienyeji kupitia fasihi.

Mwandishi huyo wa vitabu, atakumbukwa kwa kazi zake mbalimbali ambazo ziliwavutia wasomaji wengi Afrika Mashariki kama vile A Grain of Wheat, Weep Not, Child, Devil on the Cross, Wizard of the Cross na Petals of Blood.

 

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us