AFRIKA
1 dk kusoma
Watalii wawili wauawa na tembo katika hifadhi nchini Zambia
Waongozaji safari ambao walikuwa pamoja na kundi hilo walijaribu kuwazuia tembo hao kwa kuwafyatulia risasi lakini ikashindikana. Wanawake hao walifariki kwenye eneo la tukio.
Watalii wawili wauawa na tembo katika hifadhi nchini Zambia
Tembo wakiwa ndani ya hifadhi, / Reuters
4 Julai 2025

Watalii wawili wanawake watu wazima nchini Zambia waliuawa na tembo siku ya Alhamisi wakati wakitembea katika hifadhi ya taifa, polisi wamesema.

Kamishna wa Polisi wa Mkoa wa Mashariki Robertson Mweemba anasema waliouawa ni — Easton Janet Taylor, umri 68 kutoka Uingereza na Alison Jean Taylor, 67 kutoka New Zealand — walishambuliwa na tembo jike ambaye alikuwa na mtoto wake.

Waongozaji safari ambao walikuwa pamoja na kundi hilo walijaribu kuwazuia tembo hao kwa kuwafyatulia risasi lakini ikashindikana, polisi walisema.

Tembo huyo alipigwa risasi na kujeruhiwa. Waongozaji safari walishindwa kuzuia mashambulizi ya tembo na wanawake wote walifariki katika eneo la tukio, polisi walisema.

Ilifanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Luangwa Kusini mashariki mwa Zambia, karibu kilomita 600 kutoka mji mkuu, Lusaka.

Tembo jike wanalinda watoto wao sana na wanaweza kukabiliana vikali iwapo wanahisi kuna tishio.

Mwaka uliopita, watalii wawili kutoka Marekani waliuawa katika matukio tofauti ya kushambuliwa na tembo maeneo mbalimbali nchini Zambia. Katika matukio yote hayo, watalii wote walikuwa wanawake watu wazima na walikuwa kwenye gari wanalotumia kwenye safari waliposhambuliwa.

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us