30 Juni 2025
Inter wanalenga kujikatia tiketi ya robo fainali katika Kombe la dunia kwa Klabu wakati wakikabiliana na timu ya Brazil Fluminense siku ya Jumatatu.
Timu hiyo ya Flu imefuzu katika hatua hiyo ya mtoano, lakini ilimaliza nyuma ya Borussia Dortmund katika kundi F na kuingia kupambana na timu iliyocheza fainali ya Kombe la Klabu bingwa barani Ulaya.
Fluminense, imekuwa na michezo mizuri ikiwa haijafungwa katika mechi zake tisa zilizopita na walionesha makali yao walipopambana na Borussia Dortmund kwenye mechi yao ya kwanza hatua ya makundi. Mechi hiyo ilimalizika kwa sare ya kutofungana.