Rais wa Masuala ya Dini wa Uturuki ameweka kikosi cha kutosha ili kutoa huduma kwa mahujaji wa Kituruki katika kipindi hiki cha hajj kwa Waislamu.
Katika taarifa fupi kwa vyombo vya habari iliyotolewa Makkah Jumatano, mkuu wa kurugenzi Ali Erbas ametangaza kwamba Uturuki imepeleka mahujaji 84,942 nchini Saudi Arabia kwa ajili ya ibada ya Hajj ya mwaka huu.
Idadi kubwa ya mahujaji wa Uturuki tayari wamefika Makkah na Madina, na waliobaki wanatarajiwa kufika katika miji mitukufu katika siku zijazo.
Umri wa wastani wa mahujaji wa Uturuki ni miaka 60.
Erbas ameielezea ibada ya Hajj “kuwa na changamoto lakini yenye maana kubwa,” na kugusia maandalizi yaliyofanywa katika maeneo kama afya, na msaada wa fedha.
“Tunafanya uratibu wa kiwango kikubwa ili raia wetu waweze kumitiza majukumu yao ya Hajj katika njia nzuri,” amesema Erbas.
Jumla ya wanazuoni 71 na waongozaji wa kike 418 wamepelekwa kuongoza shughuli za kiroho, pamoja na viongozi wa makundi 392 na wajumbe 1,840 wakuhudumia wahujaji.
“Tunaiona ibada ya Hajji sio tu ya kiroho lakini pia safari ya kiroho na kujifunza,” amesema. “Tunataka kila hujaji arudi akiwa na uzoefu binafsi na kwa jamii.”
Maandalizi ya Arafat, moja ya vipengele muhimu kwa anayekwenda kufanya hajj, yamekamilika.
Erbas amesema mahema yenye viyoyozi tayari yamewekwa pamoja na hospitlai ya dharura kwa ajili ya kuhudumia mahujaji wagonjwa na wazee.
Ingawa muda wetu ni mfupi, pia tumeweka hospitali ya muda mfupi kwa ajili ya mahitaji ya kiafya yatakayoibuka, hasa kwa wazee wetu na mahujaji wenye changamoto za ulemavu, ambao usafiri wao utakuwa wa gari,” amesema.
Kwa kuongeza, kikosi cha Kidijitali cha Diyanet, ofisi ya waandishi wa habari, na kituo cha televisheni kipo kwa ajili ya kusaidia kutoa habari.
Ushirikiano mkubwa na Saudi Arabia
Erbas ameishukuru Saudi Arabia kwa msaada na ushirikiano wake.
“Tunafanya kazi kwa ushirikiano wa kipekee na Wizara ya Hajj ya Saudia. Kujitolea kwao kuhudumia mahujaji ni kwa kipekee, na ningependa kuwashukuru ndugu zetu katika nchi hii ya kifariki na kindugu,” amesema.