Siku ya Afrika: Rais wa Ghana aomba ushirikiano kupigania kuponya bara ili kukuza maendeleo
AFRIKA
4 dk kusoma
Siku ya Afrika: Rais wa Ghana aomba ushirikiano kupigania kuponya bara ili kukuza maendeleoKatika maadhimisho ya Siku ya Afrika 2025, Rais Mahama amewataka viongozi wenzake wa Afrika kujumuika katika kupigania kuponya majeraha ya historia ya Ukoloni Afrika, na kudai fidia na msamaha kutoka kwa mataifa yaliyohusika.
Africa Day 2025Jumapili Mei 25 ni siku ya Afrika Duniani / Others
24 Mei 2025

Wanapokusanyika mjini Addis Ababa kwa maadhimisho ya Siku ya Afrika, viongozi wa Afrika wameweka mbele suala la uponyaji wa Afrika kutoka kwa majeraha ya historia ya ukoloni na uporaji, kama msukumo muafaka wa kusonga mbele na maendeleo.

Msisitizo huu unatokana na kuwa kila bara Afrika linapojaribu kupiga hatua mbele, kuna mvuto nyuma kutokana na majeraha ambayo hayajapona au kuruhusiwa kupona yanayoambatana na historia.

Hostoria ya uporaji, ambayo kinadharia wengi wamelalama kuwa imegeuka jinamizi linalolizonga bara Afrika kulikosesha amani na uwezo wa kuangalia mbele.

Pengine ndio maana Umoja wa Afrika umeamaua kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya Afrika 2025 ni ‘Haki kwa Afrika Kupitia fidia za ukoloni’.

Makovu na majeraha yasiyopona

‘‘Kwa muda mrefu sana urithi wa utumwa, ukoloni na ukoloni mamboleo umeweka kivuli kirefu juu ya maisha na maendeleo ya Waafrika na watu wa Afrika,’’ anasema Rais wa Ghana John Dramini Mahama.

Madhila haya yamesababisha makovu kwa Waafrika au hata majeraha yasiyopona.

Lakini Rais Mahama anasema kuwa kudai fidia inaenda zaidi ya kulipwa pesa.

‘‘Fidia si tu kuhusu kutafuta kulipwa fedha bali ni kukabiliana na uharibifu mkubwa ulioletwa kwa watu wetu,’’ anasema Rais Mahama. ‘‘Zinahusu kukabiliana na ukweli japo wa kushtua, wa siku zetu zilizopita na kuchukua hatua madhubuti za kurekebisha makosa haya‘‘ anaongeza.

Jeuri la Wazungu

Lakini bila shaka hii ni mada inayowakirihi sana Wazungu wa magharibi. Hasa mataifa ambayo kihistoria yalijitajirisha kupitia ukoloni na uporaji wa mali za Afrika. Sasa kurejesha mkono wa hisani imekuwa kukamua maji kutoka kwa jiwe.

Isitoshe, mataifa hayo hayo bado ndio yamegeuka wanyama dhidi ya watu wa asili ya Afrika na wengineo waliohamia kwao kujitafutia maisha bora. Mara nyingi wanashutumiwa kuja kufyonza huduma na mali za wazungu, wengine kwa lengo la kutorejea nchi zao.

Kuna msemo wa mchekeshaji Trevor Noah, kuwa ‘‘Natamani walivyo na ukali na masuali ya kuomba viza kuingia Ulaya, babu zetu pia wangekuwa wakali hivyo hivyo walipowapokea wazee wao Afrika.’’

Ukiangalia jeuri la wazungu katika kuingilia mambo ya Afrika, na kulazimishia demokrasia yao kwa bara hili, inachekesha kwa kukumbuka mengi ya madhila yaliyoko hasa kuhusiana na mipaka na usimamizi wa rasli mali za Afrika ni wao waliosababisha.

Mkuki kwa nguruwe

Wakidai kukupa msaada, wanaweka wao masharti yake, mara nyingi ikiwemo kugawiwa migodi bila kuulizwa zaidi juu yashughuli zake. Ukikataa, wanaleta ‘Demokrasia’ kukuadhibu nayo.

Histori aimeonyesha kuwa kiongozi yeyote wa Afrika anayejaribu kuweka watu wake kwanza, anatafutiwa njia za kuondolewa au kupinduliwa na kubandikwa kila aina na kashfa. Lakini wao wazungu wana haki ya kuamua ghafla kuwafurusha Waafrika hata waliokuwa huko kama wanafunzi wa vyuo, kwasababu, nchi yao inakuja kwanza.

Kumbe mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu.

Lakini tukirudi kwa kurekebisha makosa ya kale, Rais Mahama anataka utambulisho wa makosa, ulipaji fidia na ikiwezekana kuombwa msamaha kwa Waafrika na maaifa yaliyojiajirisha kupitia rasli mali walizopora au hata biashara ya utumwa waliojifaidi nayo.

Vito vya thamani vilivyoibwa

Lakini pia lazima utenda kazi na uhusiano kwenda mbele ubadilike.

‘‘Lazima tushughulikie mzigo wa madeni unaoendelea kudumaza ukuaji wa uchumi katika mataifa mengi ya Afrika, matokeo ya moja kwa moja ya unyonyaji na mazoea ya biashara isiyo ya haki kwa pande zote,’’ anasema Rais Mahama.

Rais Mahama pia amegusia suala la kurejeshwa kwa vito vya thamani vilivyoibwa kutoka Afrika.

Japo katika miaka miwili hivi tumeona baadhi ya nchi zimekubali kurejesha baadhi ya vito, ni ton etu katika bahari ukilinganisha na mamilioni ya vito vilivyotapakaa katika vyumba vya kumbukumbu kote ulaya.

Uharibifu wenyewe

Lakini hili limepata pingamizi za wazi kabisa kutoka kwa wengi wa wasimamizi wa vyumba vya kumbukumbu Ulaya wakidai kuwa Waafrika hawana uwezo wa kuifadhi vito hivyo na kuwa wataviharibu.

Kabla ya kuwarushia jibu la hasira, Waafrika wanatakiwa wajiulize ukweli katika hili.

Mfano nchini Sudan, via vimekuwa vikiendelea kwa zaidi ya mwaka mmoja. Cha kuhuzunisha ni kuwa, pande zote mbili zinazo zozana zimeshutumiwa kuvamia, kupora na hata kuchoma hifadhi muhimu na vito vya thamani.

Pengine kuna haja ya kuweka taasisi zenye nguvu zitakazo simamia na kulinda rasli mali hizi chini ya Umoja wa Afrika kuhakikisha bila, kuegemea upande wowote, chochote kinachoendelea kisiasa katika nchi za Afrika, haziathiri historia na mali zake asili.

Viongozi kusimama pamoja

Lakini hata kama Afrika ni waharibifu, wanaharakati wanasema hiyo sio sababu ya kuwapokonya haki yao na mali zao.

Kuendana na kauli mbiu ya 2025, Rais Mahama amewataka viongozi wengine wote wasimame pamoja katika kupigania haki na mali za Afrika zilizoporwa akisema ndio njia pekee ya kusonga mbele.

‘‘Acha juhudi zetu za kupigania fidia ziwe ushuhuda wa uthabiti wetu azimio letu na imani yetu isiyoyumba katika mustakabali mzuri.’’

CHANZO:TRT Afrika Swahili
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us