AFRIKA
1 dk kusoma
Rais wa zamani wa DRC Joseph Kabila arudi nchini humo kupitia Goma
Licha ya kuondoka nchini humo mwaka 2023, kiongozi huyo bado ana ushawishi mkubwa nchini DRC.
Rais wa zamani wa DRC Joseph Kabila arudi nchini humo kupitia Goma
Kwa muda mrefu sasa, Rais wa DRC Felix Tshisekedi, amekuwa akimtuhumu Kabila kwa nyuma ya waasi hao./Picha:Wengine
29 Mei 2025

Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Joseph Kabila amerejea nchini siku ya Alhamisi kupitia jiji la Goma, linaloshikiliwa na waasi wa M23.

Ujio wa Kabila nchini DRC unakuja wakati kiongozi huyo akikabiliwa na tuhuma za uhaini kwa tuhuma za kuwaunga mkono M23.

Kwa muda mrefu sasa, Rais wa DRC Felix Tshisekedi, amekuwa akimtuhumu Kabila kwa nyuma ya waasi hao.

Timu ya wanahabari wa AFP, ilimwona Kabila akifanya mazungumzo na viongozi wa dini mbele ya msemaji wa M23, Lawrence Kanyuka.

Licha ya kuondoka nchini humo mwaka 2023, kiongozi huyo bado ana ushawishi mkubwa nchini DRC.

Ujio wa Kabila mwenye umri wa miaka 53, unakuja baada ya chama tawala nchini humo kumuonya akae mbali na siasa za nchi hiyo.

 

CHANZO:AFP
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us