Kimnyole Arap Turukat alikuwa ni kiongozi wa kiroho wa nne, katika jamii ya Wanandi wa nchini Kenya, mwanzoni mwa miaka ya 1800.
Alisifika sana kwa tabiri zake, ambazo kwa kiasi kikubwa zilibadilisha maisha ya Wanandi kutoka bonde la ufa nchini Kenya.
Ingawa tarehe yake ya kuzaliwa bado haifahamiki, Kimnyole alikuwa mtoto wa Turukat na baba wa Koitalel Arap Samoei.
Alifahamika sana kwa vazi lake la ngozi ya wanyama, alilopenda kuzungushia kwenye bega lake na fimbo yake ya mkononi.
Jamii ya Wanandi ilisifika kama jeshi imara, chini ya uongozi wa Kimnyole, licha ya ugomvi wa mara kwa mara jamii ya Wamasai katika miaka ya 1870.
Hakuna kilichoharibika chini ya Kimnyole, na aliweza kuwafanya Wanandi kuwa katika ya makabila matajiri kwa idadi ya mifugo waliyoipata wakati wa mapigano.
Hata hivyo, licha ya kuwa mtabiri mzuri, Kimnyole alilaumiwa kwa kushindwa kung’amua kuhusu ugonjwa wa Sotoka, ulioathiri ng’ombe katika jamii yake, mwaka 1888.
Kilichoudhi zaidi jamii yake ni kuona ng’ombe wake kusalimika na ugonjwa huo, huku wa watu wengine wakifa.
Kutoka na gadhabu ya watu wake, Kimnyole alipigwa mawe hadi kufa mwaka 1890, hatua iliyopelekea anguko lake.
Kifo chake kiliamsha mgogoro wa urithi kati ya watoto wake, Koitalel Arap Samoei na Kipchomber Arap Koilege.
Kipchomber alishindwa katika ugomvi na kumlazimu kukimbilia Kipsigis, na kufanywa kiongozi wa kwanza wa kimila, yaani ‘Orkoiyot’.
Hata hivyo, kulikuwa na mwanzo mpya kwenye jamii ya Nandi, iliyoongozwa na Koitalel Arap Samoei