AFRIKA
1 dk kusoma
Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Kenya ajiondoa mamlakani
Baadhi ya Wakenya wamemnyooshea kidole Lagat ikidaiwa kwa kifo cha mwanablogu, Albert Ojwang’ aliyekamatwa kufuatia malalamishi ya naibu huyo aliyemshtumu kwa kumharibia jina kwenye mitandao ya kijamii.
Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Kenya ajiondoa mamlakani
Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Kenya Eliud Lagat amesema kuwa amejiondoa mamlakani kwa muda / picha: Wengine kwa X / Public domain
16 Juni 2025

Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Eliud Lagat amejiondoa katika majukumu yake ili kupisha uchunguzi kuhusu kifo cha Albert Ojwang.

Katika taarifa yake ya Juni 16, 2025, Lagat alisema hatua hiyo ilikuwa katika "mawazo mazuri na makini" kuhusu majukumu yake.

Alitaja uchunguzi unaoendelea kuhusu kifo cha Albert Ojwang, aliyekufa akiwa chini ya usimamizi wa polisi, kuwa sababu ya kuondoka ofisini kwa muda.

"Leo nimechagua kujiuzulu ... nikisubiri kukamilika kwa uchunguzi," alisema.

Baadhi ya Wakenya wamemnyooshea kidole Lagat ikidaiwa kuwa Ojwang’ alikamatwa kufuatia malalamishi ya naibu huyo aliyemshtumu kwa kumharibia jina kwenye mitandao ya kijamii.

Wakenya waliandamana Jumanne wiki iliyopita wakitaka ajiuzulu huku uchunguzi ukiendelea.

InayohusianaTRT Global - Uchunguzi waonyesha Mwanablogu Kenya aliuawa akiwa ndani ya kituo cha polisi

Lagat aliongeza kuwa naibu wake atafanya kazi za ofisi hiyo hadi uchunguzi utakapokamilika. Alionyesha nia ya kuunga mkono mchakato wa uchunguzi na akatuma risala za rambirambi kwa familia ya Ojwang.

Ojwang alifariki baada ya madai ya kushambuliwa akiwa kizuizini katika Kituo Kikuu cha Polisi, Nairobi.

Kesi hiyo imezua hasira kwa umma na kupelekea kukamatwa kwa OCS wa kituo hicho, Samson Talam.

Uchunguzi unaendelea, ukiongozwa na Mamlaka Huru ya Kusimamia Polisi (IPOA).

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us