ULIMWENGU
1 dk kusoma
Mahujaji wanakuja kutoka wapi?
Zaidi ya watu milioni 1.83 walifanya Hijja mwaka uliopita, ambapo karibu 90% walikuja kutoka nje ya Saudi Arabia. Hii ni tathmini ya mataifa gani ambayo mahujaji wa 2024 walitoka.
Mahujaji wanakuja kutoka wapi?
Mtayarishaji: Hatice Cagla Gunaydin, Mbuni wa Picha: Semih Genc / TRT World / TRT Afrika Swahili
30 Mei 2025

Mnamo mwaka wa 2024, zaidi ya watu milioni 1.83 walitekeleza ibada ya Hajj, ambapo karibu asilimia 90 ya mahujaji walitoka nje ya Saudi Arabia kupitia maeneo mbalimbali, huku idadi ya mahujaji wa ndani — wakiwemo raia na wakazi — ikifikia 221,854.

Zaidi ya nusu ya mahujaji walikuwa wanaume, huku idadi ya mahujaji wanawake ikifikia 875,027.

Maafisa nchini Saudi Arabia wanasema kuwa wanatarajia idadi ya mahujaji mwaka huu kuzidi ile ya mwaka 2024 na kufikia viwango vya kabla ya janga la UVIKO-19, wakiwa na matarajio ya watu zaidi ya milioni mbili.

Ikiwa mojawapo ya mikusanyiko mikubwa zaidi ya kidini duniani, Hajj ni moja ya nguzo tano za Uislamu. Waislamu wote wanahitajika kuitekeleza angalau mara moja maishani mwao ikiwa wana uwezo wa kufanya hivyio kiafya na kifedha.

Huu ni mchanganuo wa uwakilishi wa mabara ambayo wanatoka mahujaji waliotekeleza ibada ya Hajj 2024.

Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us