Na Charles Mgbolu
Aliko Dangote, mtu tajiri zaidi barani Afrika, siyo tu mtu maarufu katika biashara; pia ni mtu wa kuunganisha watu katika jamii.
Wiki hii, alijumuika pamoja kwa futari na mwanamuziki wa Afrobeat Burna Boy na afisa mwandamizi wa sekta hiyo Cecil Hammond akiwa na familia yake na marafiki wakati wa kupata futari.
Video imemuonesha Burna Boy akisalimiana na bilionea huyo raia wa Nigeria na watu wengine wakiwa kwenye meza kubwa wakipata futari katika siku ya nne ya Ramadhan, na mara moja ikatizamwa na watu wengi kwenye mtandao siku ya Jumatano.
Wengine pia walizungumzia kuhusu namna kujumuika kama hivyo kunaweza kuleta ushirikiano baina ya watu wa dini tofauti, ikizingatiwa kuwa mwanamuziki huyo si muislam.
Cecil Hammond, ambaye aliweka picha kwenye mtandao wake wa Instagram jioni hiyo aliandika "wakongwe pamoja, tabasamu moja baada ya lingine."
Uhusiano mzuri
Burna Boy alizindua wimbo wake ‘Dangote’ 2019 kutoka kwa albamu yake ya "African Giant."
Wimbo huo, ambao haukuwa unamzungumzia Dangote moja kwa moja, alitumia jina lake kama ishara ya ujasiri na utajiri.
Kulingana na shirika la Forbes, limemuorodhesha Dangote kama mtu tajiri zaidi barani Afrika na wa 86 kote duniani akiwa na kiasi cha dola bilioni $23.9.
Tangu kuwekwa kwa video hiyo, mashabiki wamempongeza Dangote katika mitandao ya kijamii kwa ‘‘kuunganisha’’ watu wa vizazi tofauti.
Hii siyo mara ya kwanza kwa Dangote kujumuika pamoja na watu wa sekta ya burudani. Amewahi kuonekana na watu wengine maarufu katika sekta ya muziki, ikiwa ni pamoja na mwanamuziki wa Nigeria Davido.
Hapo awali Burna Boy alikuwa katika hafla ya mfanyabiashara maarufu bilionea wa Nigeria, Femi Otedola, alijumuika pamoja na Burna Boy, Hammond, na Wizkid nyumbani kwake Jumatano, 28 Februari, kwa kile walichokiita mazungumzo ya biashara wakati wakipata chakula cha usiku.