ULIMWENGU
2 DK KUSOMA
DRC: Jeshi la Kongo lataka ushirikiano wa raia ili kuwadhibiti wanamgambo
Jeshi la Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo lataka ushirikiano na wananchi siku tatu baada ya shambulizi lililopelekea mauaji ya watu 23
DRC: Jeshi la Kongo lataka ushirikiano wa raia ili kuwadhibiti wanamgambo
Wakati maridhiano yakiendelea kutafutwa wanamgambo washambulia Ituri / Picha: Reuters
22 Machi 2023

Pamoja na jitihada za jumuia ya Afrika mashariki kumaliza mgogoro na vurugu ambazo zimekuwa zikiendelea katika Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo hali bado ni si shwari.

Kufuatia ripoti ya mauaji ya watu 23 mashariki mwa Kongo, jeshi la Congo limewataka raia kutoa ushirikiano ili kumaliza vita mashariki mwa Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo.

“Nawataka raia kuwa na subira pia nasisitiza uhusiano kati yetu na raia—watu wanatakiwa kupiga simu kwa jeshi la Kongo wakiona hao maadui lakini hawakutoa taarifa. Jeshi la Congo linaendelea kuwa saka hao maadui" anasema kanali Jacques Disanoa

Kwenye mazungumzo na TRT Afrika kanali Disanoa anasisitiza kuwa "Raia wanatakiwa kutuamini” huku akithibitisha vifo vya takribani watu 27 kwenye kwenye shambulizi la jumamosi.

Wanamgambo wa CODECO walivaamia kijiji cha Panduru kwenye jimbo ya Ituri kaskazini mashariki mwa Kongo siku ya jumapili na kuwasha moto kwenye makazi ya raia.

Kwa sasa idadi ya watu waliofariki huenda ikaongezeka —Askari jeshi na raia waendelea kutafuta miili ya watu waliofariki.

TRT Afrika imeongea na baadhi ya wakazi wa maeneo hayo na wanasema kuwa waliwaona watu waliovaa sare za kiaskari na silaha mkononi wakishambulia eneo lao na kuwasha moto kwenye makazi yao.

"Nilifanikiwa kukimbia. Nimetembea kilomita nyingi kabla nifike mji wa Bunia. Nimeona miili ya watu walio uwawa. Ahsante Mungu mimi na familia yangu tuko salama hapa Bunia’’ Innocent Webekudu ameambia TRT Afrika

Shirika la Umoja wa mataifa linalo husika na wakimbizi lasema watu takribani milioni moja na nusu wamekimbia makazi yao kwenye eneo la Ituri kuanzia Oktoba 2022.

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us