Mwanamuziki nyota wa reggae kutoka Jamaica Cocoa Tea amefariki dunia nchini jijini Florida nchini Marekani.
Cocoa Tea, ambaye jina lake halisi ni Colvin Scott amefariki kwa mshtuko wa moyo wakati akiwa hospitali siku ya Machi 11, 2025, kulingana na mkewe Malvia Scott.
Cocoa Tea, ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 65, atakumbukwa kwa nyimbo zake maarufu kama vile 18 and Over (Young Lover) na Hurry Up and Come.
Akitoa salamu zake za rambirambi, Waziri Mkuu wa Jamaica Andrew Holness, alisema muziki wa Cocoa Tea ulikuwa na ushawishi mkubwa ukivuka mipaka, kugusa mioyo ya watu na kuiweka Jamaica kwenye ramani ya muziki ulimwenguni.
“Mbali na umahiri kwenye muziki, Cocoa Tea alikuwa ni ishara ya ukarimu akiwainua watu wa chini…tunapoendelea kuomboleza kifo chake, ni vyema kuenzi na kufurahia urithi aliotuachia,” aliongeza.