AFRIKA
1 DK KUSOMA
Miss Rwanda 2022 Divine Muheto kupandishwa mahakamani
Mlimbwende huyo anashikiliwa na vyombo vya sheria kwa makosa mbalimbali, ikiwemo kuendesha gari bila ya kuwa na leseni.
Miss Rwanda 2022 Divine Muheto kupandishwa mahakamani
Muheto alishinda taji la Miss Rwanda mwaka 2022./Picha: Wengine / Others
30 Oktoba 2024

Mahakama ya Mwanzo ya wilaya ya Kicukiro nchini Rwanda, siku ya Oktoba 31 itasikiliza shauri dhidi ya Miss Rwanda 2022, Divine Nshuti Muheto.

Kulingana na msemaji wa ofisi ya taifa ya mwendesha mashtaka nchini Rwanda (NPPA) Faustin Nkusi, jalada la kesi hiyo tayari limefikishwa kwenye Mahamaka ya Mwanzo ya Kicukiro kwa ajili ya kusikilizwa siku ya Oktoba 31.

Jeshi la Polisi nchini Rwanda, lilithibitisha kukamatwa kwa mlimbwende huyo kwa kosa la kuendesha gari bila kuwa na leseni huku akiwa ametumia kilevi na kusababisha uharibifu wa miondombinu.

Hata hivyo, hii si mara ya kwanza kwa Muheto kuhusika na matukio ya aina hiyo, polisi walisema kupitia mtandao wao wa X.

Muheto alishinda taji la Miss Rwanda mwaka 2022.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us