AFRIKA
2 dk kusoma
Diamond Platnumz: Mfalme wa Muziki wa Bongo na dhahabu yake ya YouTube milioni 10
Wakati wakali wengine wa Afrobeats wakijivunia namba za kuvutia, Diamond Platnumz kwa sasa yuko kwenye ligi ya aina yake, akionyesha ubabe wake wa kidijitali usio na kifani.
Diamond Platnumz: Mfalme wa Muziki wa Bongo na dhahabu yake ya YouTube milioni 10
Doamond platinumz wa Tanzania amewashukuru mashabiki wake kwa kumfikisha zaidi ya milioni 10 kwa You Tube/ Picha: Wengine / Others
3 Julai 2025

Diamond Platnumz wa Tanzania amevunja rekodi, na kuwa msanii wa kwanza wa Kiafrika kufikisha watu milioni 10 wanaomfuatilia kupitia YouTube.

Ili kuadhimisha mafanikio haya, mwimbaji wa kibao cha "Gere" alipewa Kitufe cha almasi kinachotamaniwa, zawadi adimu na ya kumeta iliyohifadhiwa kwa watayarishaji wanaofikia hatua hii ya kipekee.

"Diamond Platinumz milioni, tunataka kukupa hii... ( heshima kubwa ) Respect, man...respect," alisema mwakilishi wa YouTube kwenye video ya uwasilishaji iliyoshirikiwa na Diamond kwenye Instagram.

Diamond mwenye furaha alishukuru jukwaa la kushiriki video la YouTube kwa "kubadilisha maisha yangu" na kujitolea kwa mashabiki wake.

Kazi ngumu

"Ni kazi nyingi sana, jamani... Ni kibao cha almasi kwa Diamond Platnumz. Kwanza nataka kuweka wakfu hii kwa mashabiki wangu, watazamaji wangu. Timu yangu, familia, kila mtu katika tasnia," alisema.

Diamond pia alitumia Instagram kuonyesha furaha na kutoa shukrani zake:

"Asante, YouTube, mashabiki wangu, timu yangu na familia yangu! Wasajili Milioni 10 na zaidi kwenye YouTube"

Hatua hii ni uthibitisho wa kukua kwa nguvu na ufikiaji wa sanaa ya Kiafrika.

Wakati wakali wengine wa Afrobeats wakijivunia namba za kuvutia, Diamond Platnumz kwa sasa yuko kwenye ligi ya aina yake, akionyesha ubabe wake wa kidijitali usio na kifani.

Burna Boy aliyeshinda tuzo nyingi za Grammy, nguli wa Nigeria, anajisajili kwa watumiaji milioni 5.43 wa YouTube, na mwanamuziki wa Nigeria aliyevunja rekodi ya Guinness Rema ana milioni 4.97.

Mshindi wa tuzo za Grammy nchini Afrika Kusini, Tyla amejinyakulia milioni 4.88, huku Davido wa Nigeria akishinda milioni 4.59.

Msanii mwenyewe

Diamond Platnumz , ikiwa jina halisi Naseeb Abdul Juma Issack, alizaliwa tarehe 2 Oktoba 1989, Tandale, eneo dogo la Dar es Salaam, Tanzania .

Alikabiliwa na changamoto za kiuchumi.

Mafanikio yake yalifika mwaka wa 2010 na kibao kikali cha "Kamwambie", kilichofuatiwa haraka na uteuzi wa Msanii Bora Mpya katika Tuzo za Muziki za MTV Afrika huko Lagos, Nigeria, mwaka huo huo.

Kuanzia hapo, nyota yake iliendelea kupanda kwa safu ya juu-chati, zikiwemo "Number One", "Jeje", "Waah", "Inama", na "Yope".

Ingawa lugha yake kuu ya muziki ni Kiswahili, mchanganyiko wake wa kipekee wa Bongo Flava na sauti nyingine za Kiafrika umewavutia mashabiki mbali zaidi ya mipaka ya bara hili.

Kabati lake la kombe pia limejaa sifa kutoka kwa mashirika maarufu ya tuzo, pamoja na Tuzo za Muziki za MTV, tuzo za Channel O na AFRIMA, miongoni mwa zingine.

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us