Machafuko ya kikatili yanayozidi kuongezeka yanaifikisha Haiti "pabaya", maafisa waandamizi wa Umoja wa Mataifa wameonya Baraza la Usalama la umoja wa Mataifa.
Magenge yanaripotiwa kuendeleza udhibiti wao katika nchi hiyo na kuongeza hatari ya kusambaratika kabisa kwa serikali katika mji mkuu.
Baraza la Muda la Uchaguzi, likiungwa mkono na Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Haiti (BINUH), limeendelea na maandalizi ya kufanya uchaguzi ndani ya muda uliowekwa na makubaliano ya Aprili 2024.
Hata hivyo, ucheleweshaji wowote au juhudi za kudhoofisha mchakato wa mpito wa kisiasa kufikia tarehe ya mwisho iliyowekwa ya 7 Februari 2026 ya kuweka uongozi mpya uliochaguliwa hivi karibuni na bunge ni jambo linalozua wasiwasi mkubwa.
"Haiti haina uwezo wa kuhimili mabadiliko ya kisiasa," alisema Miroslav Jenča, Katibu Mkuu Msaidizi wa Ulaya, Asia ya Kati na Amerika, Idara za Masuala ya Kisiasa na Kuimarisha Amani na Operesheni za Amani.
Haiti imegawanywa kiutawala katika maeneo kumi.
“ Wakati huo huo, mashambulizi makubwa katika maeneo ya Artibonite na Centre, hasa Mirebalais, yanaonyesha uwezo na nia ya magenge kupanua wigo wao..” aliongeza.
Akisikitishwa na "ukatili na ukubwa wa ghasia", alibainisha kuwa mwaka huu pekee BINUH ilirekodi mauaji ya kukusudia ya watu 4,026 - ongezeko la asilimia 24 kutoka kipindi kama hicho mwaka jana - na wakimbizi wa ndani milioni 1.3, "idadi nyingine mbaya ya kumbukumbu".
Mkutano huo wa UN umesema kuwa kwasababu ya uwezo mdogo wa ulinzi wa Serikali, vikundi vya kujilinda vinapata ujasiri zaidi.
Licha ya kuendelea kutoripoti unyanyasaji wa kingono, BINUH ilirekodi matukio 364 yaliyohusisha waathirika 378 kuanzia Machi hadi Aprili.
Aliripoti kwamba ujumbe wa Kimataifa wa Kusaidia kuleta Usalama unaoongozwa na Kenya na Polisi wa Haiti umeshindwa kupiga hatua katika kurejesha mamlaka ya Serikali.
“ Bila msaada wa ziada kutoka kwa jumuiya ya kimataifa, hali ni mbaya,” alisema.
Mjumbe wa Kenya katika mkutano huo wa UN alieleza kuwa 25 Juni iliadhimisha mwaka mmoja tangu nchi yake kupeleka kikosi cha kwanza cha Ujumbe wa Kimataifa wa kusaidia kuleta Usalama nchini Haiti, akisema kwa sasa kuna maafisa 991.
Hata hivyo, hii ni chini ya mpango wa kikosi kuwa na maafisa 2,500.