AFRIKA
1 dk kusoma
Trump kuwa mwenyeji wa viongozi watano wa Afrika wiki ijayo - taarifa
Viongozi kutoka Gabon, Guinea-Bissau, Liberia, Mauritania na Senegal wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo jijini Washington, kwa mujibu wa taarifa.
Trump kuwa mwenyeji wa viongozi watano wa Afrika wiki ijayo - taarifa
Rais wa Marekani Trump wakati akiwa na mawaziri wa mambo ya nje wa Rwanda na DRC katika Ikulu ya Marekani. / Reuters
3 Julai 2025

Kongamano la kwanza la Viongozi wa Afrika katika muhula wa pili wa Rais wa Marekani Donald Trump litafanyika wiki ijayo jijini Washington, huku wakuu wa nchi kutoka mataifa ya Afrika ya kati na magharibi wakitarajiwa, vyombo vya habari vilitoa taarifa siku ya Jumatano.

Mkutano huo utafanyika kuanzia Julai 9-11 na utahudhuriwa na Trump pamoja na viongozi wa Gabon, Guinea-Bissau, Liberia, Mauritania na Senegal, kwa mujibu wa taarifa.

Kusitishwa kwa misaada ya kigeni

Serikali ya Trump imepunguza kwa kiasi kikubwa misaada ya Marekani kwa mataifa ya Afrika ikiwa ni sehemu ya mpango wa kupunguza matumizi ambayo wanaona ni ubadhirifu na yasiyoendana na sera ya Trump ya "Marekani Kwanza".

Taarifa hio inasema kuwa inataka kuangazia zaidi biashara na uwekezaji pamoja na kuimarisha maendeleo kwa faida ya mataifa yote.

Siku ya Jumanne, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio alisema kuwa Marekani inaachana na mfumo wa kutoa misaada na itashirikiana na yale mataifa ambayo yanaonesha "nia na ari ya kujisaidia wenyewe".

Mabalozi wa Marekani barani Afrika watapimwa kwa namna watakavyovutia miradi ya biashara, Afisa mwandamizi wa idara ya masuala ya Afrika ya Marekani Troy Fitrel alisema mwezi Mei, akieleza kuwa ni mkakati mpya wa misaada kwa bara hilo.

Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us