AFRIKA
3 dk kusoma
Mwanablogu Kenya aliyedhaniwa kutekwa nyara ajitokeza
Kumekuwa na mjadala Kenya iwapo Mwanablogu huyo alitekwa nyara na maafisa wa usalama au alidhamiria kujificha.
Mwanablogu Kenya aliyedhaniwa kutekwa nyara ajitokeza
Wakili wa Kinyagia ameomba mahakama kumpa wiki moja kuzungumza na familia yake akisema mwanaharakati anaonekana kuwa na kiwewe/ picha: Wengine / Public domain
3 Julai 2025

Kumekuwa na hali ya kutoelewana nchini Kenya wakati mwanablogu Ndiangui Kinyagia ambaye aliripotiwa kutekwa nyara alipojitokeza mahakamani jijini Nairobi.

Mahakama Kuu, Juni mosi iliamuru maafisa wa kitengo cha jinai, DCI kumleta kijana huyo wakati huo huo akimtaka mkuu wa DCI kujiwakilisha mahakamani 3 Julai 2025.

Mama yake aliangua kilio huku akimkumbatia mwanae ambaye alitoweka kwa zaidi ya wiki moja sasa.

Ndiangui aliingia katika chumba cha mahakama akisindikizwa na mawakili Kibe Mungai na wakili mkuu Martha Karua.

Jaji Chacha Mwita Jumanne aliagiza mwanablogu huyo kufikishwa mahakamani akiwa hai au amefariki.

Wahome Thuku, wakili wa familia, alifichua jambo la kushangaza akidai kuwa mwanablogu huyo aliyetoweka alikuwa amejificha katika eneo lisilojulikana.

“Mimi ndiye niliyechapisha na kutangaza habari za Ndiangui Kinyagia kwenye vyombo vya habari, ili zitoke kwa jamaa na sio kupitia fununu,” Thuku aliwaambia waandishi wa habari.

Mwanablogu huyo aliripotiwa akisema kuwa yuko tayari kujiwasilisha kwa DCI na kufika mbele ya mahakama ya sheria, lakini baada ya usalama wake kuhakikishiwa.

“DCI imethibitisha mahakamani kwamba walienda nyumbani kwake mara mbili saa mbili usiku na 11 jioni na kuingia kwa nguvu. Yeyote anayedai kuwa hii ilikuwa kesi ya kujiteka nyara anapaswa kueleza ikiwa DCI kuvamia nyumba yake ilikuwa sehemu ya utekaji nyara huo,” aliongezea.

Thuku aliandika katika akaunti yake ya mitandao kuwa “Ndiangui ambaye alitoweka wiki jana amewasiliana na familia na kwamba ni mzima, mwenye afya njema na yuko salama.”

Aliongezea kuwa “Ndiangui aliwasiliana na mwanafamilia Jumanne jioni kutoka eneo lisilojulikana. Ndiangui alimweleza mwanafamilia huyo kuwa alikuwa amejificha kwa muda kwa kuhofia maisha yake alipojua kwamba maafisa wa DCI walikuwa wakimsaka kwa madai ya uhalifu yasiyojulikana.”

Kampeni mitandaoni na katika vyombo vya habari kwa siku kadhaa zimekuwa zikiinyoshea kidole kitengo cha makosa ya jinai, DCI.

Wakili huyo aliongeza kuwa Kinyagia "alijificha kwa muda kwa kuhofia maisha yake baada ya kujua kwamba maafisa wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) walikuwa wakimsaka kutokana na tuhuma zisizojulikana za uhalifu."

Wakili huyo aliongeza kuwa Kinyagia "alijificha kwa muda kwa kuhofia maisha yake baada ya kujua kwamba maafisa wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) walikuwa wakimsaka kutokana na tuhuma zisizojulikana za uhalifu."

Habari za kudaiwa kujificha kwa Ndiangui zilipokelewa kwa njia tofauti na baadhi ya Wakenya, huku wengi wakimsuta kwa kucheza michezo ya kiakili na taifa huku wengine wakitilia shaka simulizi hiyo, wakiamini kuwa hadithi ya uongo iliyowasilishwa na DCI na Ndiangui kulazimishwa kubuni kuwa ni ukweli.

Jaji wa Mahakama Kuu Chacha Mwita alisema anangoja uamuzi wa mawakili kama wanataka kesi kuendelea.

“Nafikiri jambo la haki ni kuruhusu familia na wewe mwanasheria mzungumze kisha muamue jinsi ya kuendelea. Nia yangu asubuhi ya leo ilikuwa kumuona Ndiangui Kinyagia na kumwasilisha kwa Wakenya akiwa hai na nimefanya hivyo. Kitu chengine chochote kinakuja baada ya uamuzi wenu,” Jaji Mwita alisema.

Wakili Kibe Mungai anaomba Mahakama kumpa Ndiangui Kinyagia wiki moja kuzungumza na familia yake kwa ‘kujiamini,’ anasema mwanaharakati anaonekana kuwa na kiwewe.

Mahakama imeipa familia ya Ndiangui Kinyagia muda wa kumpeleka hospitali kwa matibabu.

Kesi hii itasikilizwa tarehe 18 na 24 Julai saa nne unusu alfajiri.

“Wakati huo huo, polisi hawatamkamata Ndiangui Kinyagia, kwa kuwa sasa ni mtu wa dhamana katika suala hili na anaweza kuhitajika kutoa ushahidi. Ikibidi, anaweza kuwasilishwa kwa DCI ili kurekodi taarifa, lakini hatakiwi kukamatwa au kuzuiliwa,” Jaji Chacha amesema.

CHANZO:TRT Swahili
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us