AFRIKA
1 dk kusoma
Idadi ya waliofariki katika ajali ya maboti 2 ya abiria DRC imefika 52
'Ajali hiyo imesababishwa na watu kujaa zaidi ya inavyotakiwa na upepo mkali huku kukiwa na mvua mkubwa,' alisema afisa mmoja
Idadi ya waliofariki katika ajali ya maboti 2 ya abiria DRC imefika 52
13 Juni 2025

Watu wasiopungua 52 wamethibitishwa kufariki,na wengine kadhaa hawajulikani waliko baada ya maboti mawili ya abiria kupata ajali katika Ziwa Tumba magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, maafisa walisema siku ya Ijumaa.

Maboti haya yalizama usiku wa kati ya Jumatano na Alhamisi karibu na Bikoro,kilomita 128 kutoka Mbandaka mkoa wa Equateur.

Dieu Merci Akula Mboyo, afisa mmoja wa shirika la kijamii katika mkoa huo, amesema kwa sasa idadi ya waliothibitishwa kufariki ni 52.

“Ajali hiyo ilisababishwa na abiria kujaa zaidi ya inavyotakiwa na upepo mkali huku kukiwa na mvua,” Mboyo aliwaambia waandishi wa habari huko Bikoro.

Aliongeza kuwa awali wasimamizi wa maboti hayo walikataa kuchukuwa abiria zaidi lakini baadaye wakazidiwa nguvu.

Mboyo alitaka serikali ifanye uchunguzi wa kina kubaini nani amehusika na kuepuka ajali kama hizo katika siku zijazo.

Mapema siku ya Alhamisi, Waziri wa mambo ya ndani wa mkoa Chrispin Moliy anasema serikali zote za mkoa na kitaifa zitahakikisha kuwa mazishi yanafanyika kwa miili itakayopatikana.

Idadi kamili ya wale ambao hawajapatikana haijathibitishwa na mamlaka, lakini vyombo vya habari vinakadiria kuwa kuna watu karibu 100 waliokuwa kwenye maboti hayo.

Maboti hayo yalikuwa yanasafiri kutoka Bikoro hadi katika gulio la kijiji cha karibu yalipozama wakati wa dhoruba hiyo.

CHANZO:AA
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us