AFRIKA
2 dk kusoma
Rais wa Afrika Kusini atembelea eneo lililokumbwa na mafuriko mabaya
Ziara ya rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa inakuja huku mamlaka zikalaumiwa' kuhusu kusuwasuwa kwake katika kukabiliana na janga hilo, ambalo lilisababishwa na hali mbaya ya hewa iliyoleta mvua kubwa, upepo mkali na hata theluji.
Rais wa Afrika Kusini atembelea eneo lililokumbwa na mafuriko mabaya
Rais Cyril Ramaphosa ametembelea daraja la la eFata huko Mthatha ambapo basi la shule lilisombwa na mafuriko. / Wengine
13 Juni 2025

Siku ya Ijumaa rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alitembelea maeneo yaliyokumbwa na mafuriko yaliyosababisha vifo vya watu wasiopungua 78 kusini mashariki mwa nchi huku juhudi za uokoaji zikiendelea kwa siku ya nne na mamlaka zikisema kuwa huenda idadi ya waliofariki ikaongezeka.

Ramaphosa amesafiri hadi katika mji wa Mthatha mkoa wa Eastern Cape, ambapo mafuriko yalikuwa hatari zaidi, na kutembelea daraja ambalo basi la shule lilisombwa na maji na kusababisha vifo vya wanafunzi kufuatia mvua kubwa siku ya Jumanne.

Watabiri wa hali ya hewa walionya kuhusu hali hiyo mbaya ya hewa ya wiki iliyopita.

Hamna vifaa vya kutosha

Mkuu wa serikali ya mkoa amesema juhudi za uokoaji “zilikwama’’ katika saa chache za kwanza baada ya mafuriko kwa sababu hakukuwa na vifaa maalum kwa ajili ya uokoaji, waogeleaji na mbwa wa K-9 katika moja ya maeneo yenye umaskini mkubwa nchini.

Waziri Mkuu wa mkoa wa Eastern Cape Oscar Mabuyane anasema mkoa huo wa idadi ya watu milioni 7.2 una helikopta moja tu rasmi ya uokoaji, ambayo ilibidi iletwe kutoka mji mwingine zaidi ya kilomita 500 kutoka hapo.

‘Watu kufariki’

“Nahitaji msaada wa kisaikolojia kwa sababu nimeona watu wakifariki mbele ya macho yangu. Walikuwa wanavutwa kutoka kwenye maji wakiwa juu ya mabati," amesema Zinathi Vuso, mkazi wa Mthatha.

"Wengine walijaribu kushikilia kifaa chochote, lakini vilikuwa vinavunjika na hatimaye wakafariki. Ndiyo maana unaona miili inaendelea kuolewa na wengine bado hawajapatikana.”

Waziri wa Vyama vya Ushirika na masuala ya Kitamaduni Velenkosini Hlabisa, ambaye aliongoza maafisa wa serikali ya kitaifa waliopelekwa katika mkoa huo mwanzoni mwa wiki, alisema kupitia televisheni ya taifa ya shirika la habari la SABC siku ya Alhamisi kuwa mamlaka zimetoa wito kwa wakazi kuwapa taarifa za watu ambao hawajapatikana ili waokoaji wajuwe ni watu wangapi ambao bado wanatakiwa kuwatafuta.

“Tuna tatizo kubwa. Janga la kikweli,” Hlabisa alisema. “Na pindi maji yanapotulia, miili zaidi inapatikana.”

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us