Ladoum ni aina ya kondoo mwenye thamani kubwa Senegal, aliye
na gharama kubwa kabisa duniani.
Aina hiyo ya kondoo wa Ladoum aliye bora Senegal alichaguliwa katika mashindano yaliyofanyika katika Maonyesho ya Kimataifa ya Mifumo Dakar. Waamuzi walipima wanyama 18 katika mashindano: urefu, uzito, upana wa kifua, na urefu wa mgongo.
Mshindi alikuwa ni “Niang Ballo,” ambae alikuwa na uzito wa kilo 156.Kondoo aina ya Ladoums mara nyingi hawachinjwi.
Wanafugwa sana katika maeneo ya mijini, na wanauzwa wakiwa na taarifa zao kamili na idadi ya tuzo walizoshinda katika mashindano.Hiki ni kizazi cha fahari. Baadhi ya wanyama wana majina kama vile “Maison Blanche,” “Hamilton,” “Ronaldo,” “Rambo,” “Sankara,” na “Cleopatra.”
Hata wana wafuasi wao katika kurasa za Facebook.Nchini Senegal, “Ladoum Galactique” mwenye gharama ya juu kabisa aliuzwa kwa kiasi cha dola 90,000, au CFA milioni 51.Ladoum Galactique pia ana ukurasa wake maalumu wa TikTok.