AFRIKA
1 dk kusoma
Waasi wa M23 wataka mazungumzo zaidi ya amani DRC licha ya kusainiwa kwa mkataba wa Washington
Kulingana na kikundi hicho, bado ipo haja ya kufanya mazungumzo mengine ili kutatua baadhi ya matatizo ambayo bado yanaendelea kuchochea mgogoro Mashariki mwa DRC.
Waasi wa M23 wataka mazungumzo zaidi ya amani DRC licha ya kusainiwa kwa mkataba wa Washington
Waasi wa M23./Picha:Getty
3 Julai 2025

Kikundi cha waasi wa M2 kimesisitiza haja ya kuwa na mazungumzo mengine ya amani ya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, licha ya mkataba wa amani kati ya Rwanda na DRC, uliotiwa saini Juni 27, jijini Washington nchini Marekani.

Kulingana na kikundi hicho, bado ipo haja ya kufanya mazungumzo mengine ili kutatua baadhi ya matatizo ambayo bado yanaendelea kuchochea mgogoro Mashariki mwa DRC.

"Kinachotokea kati ya DRC na Rwanda kinahusu nchi hizo mbili tu,” alisema Katibu Mtendaji wa M23, Benjamin Mbonimpa katika mkutano wake na waandishi wa habari siku ya Alhamisi.

"Matatizo yetu hayakujadiliwa kwenye mkataba uliosainiwa jijini Washington."

Toka kuanza kwa machafuko hayo mwanzoni mwa mwaka 2025, waasi wa M23 wametwaa na kudhibiti maeneo muhimu ya eneo la mashariki mwa DRC, ikiwemo Goma na Bukavu.

Kwa upande mwingine, nchi Rwanda imekaan madai ya kuhusika na machafuko hayo, licha ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa, kusisitiza kuwa nchi hiyo ilihusika pakubwa kwa kutoa misaada ya kijeshi kwa waasi wa M23.

Wakati huo huo, Rais Paul Kagame wa Rwanda na mwenzake wa DRC Felix Tshisekedi, wanatarajiwa kukutana miezi michache ijayo, kama ishara ya kuongezea nguvu mazungumzo hayo ya Washington.

CHANZO:AFP
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us