Na Pauline Odhiambo
Steven Ogallo anatumia utaalamu wake kuchora picha mbalimbali zenye kuibua hisia.
"Nilisomea ubunifu kurasa lakini nikapa kazi ya kuhariri picha,” anaiambia TRT Afrika.
“Ila nilivutiwa zaidi na upigaji picha lakini kama sio kazi hiyo, sidhani kama ningekuwa mpiga picha leo."
Hata hivyo, kama bahati, akajikuta akijifunza mbinu za upigaji picha, ikiwemo kuzisafisha.
Kitu cha ghafla
"Niliifanya kazi hiyo kwa muda wa miaka mitatu lakini nikajiongeza zaidi," anasema.
Hata hivyo, kama bahati, akajikuta akijifunza mbinu za upigaji picha, ikiwemo kuzisafisha./Picha: Steven Ogallo
Mara kwa mara, amekuwa akifanya katika tasnia ya mavazi huku kazi zake zikiwa zinatawala.
"Mchakato wa uchoraji ni kitu cha papo kwa hapo. Huwa naanza na kile kinachokuja akilini mwangu,” anasema.
Uchoraji wa mwilini
"Wale ninaowachora huwa kama maktaba zinazotembea," anaongeza.
Mpiga picha huyo hufanya kazi na wajasiriamali wengi wenye kutegemea uwezo wake katika kuinua biashara zao. Ujuzi wake pia hutumika katika kutengeneza matangazo.
Ujuzi wake huhusisha uongozaji wa upigaji picha na kuwaelekeza waonesha mavazi./Picha:Steven Ogallo
Ujuzi wake huhusisha uongozaji wa upigaji picha na kuwaelekeza waonesha mavazi.
"Huwezi kumlazimisha mtu kwenda zaidi ya uwezo wake, na ndio maana huwa nawaelekeza waonesha mavazi kuendana na uhalisia wao," anaeleza.
“Lakini hatua ya kwanza ni kuwa na wazo, kuliendeleza hilo wazo kwa kutumia watu sahihi watakaovaa uhusika huo."
Kwa sababu hii, Ogallo hupendelea kufanya kazi na waonesha mavazi wazoefu ambao huvaa uhusika kwa usahihi wawapo mbele ya kamera.
Kwa sababu hii, Ogallo hupendelea kufanya kazi na waonesha mavazi wazoefu ambao huvaa uhusika kwa usahihi wawapo mbele ya kamera./Picha: Steven Ogallo
Licha ya kuwa na ujuzi wa kawaida wa vifaa vya kupiga picha, Ogallo ni muumini wa uongezaji wa ujuzi. "Ninapenda kusoma juu ya upigaji picha kwa sababu ninaamini sana katika elimu. Hapo awali nilipata maarifa yangu kwenye mtandao kwa kupakua video za upigaji picha na mafunzo pamoja na miongozo mingine."
Haijawa rahisi kwa Ogallo kujigawa katika majukumu yake hayo.
Hata hivyo huhamasika na kuwatia moyo wapiga picha wanaochipukia wenye kumtazama yeye kama mfano.