AFRIKA
1 dk kusoma
Rais wa Zanzibar azindua nembo ya 'Made in Tanzania'
Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi anasema nembo hiyo itachochea kuimarisha biashara na kukuza uzalendo pamoja na kuwahimiza Watanzania kuunga mkono juhudi za kununua bidhaa zinazotengenezwa nyumbani.
Rais wa Zanzibar azindua nembo ya 'Made in Tanzania'
Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi azinduwa nembo ya 'Made in Tanzania'. / Picha:Ikulu Zanzibar
tokea masaa 11

Tanzania imezindua rasmi nembo ya ‘Made in Tanzania’ kwa lengo na kutangaza bidhaa zinazotengenezwa nyumbani kimataifa na kuitangaza Tanzania kama nchi ambayo inatengeneza bidhaa zenye ubora wa hali ya juu, ubunifu na hasa zenye asili ya Kiafrika.

Nembo hiyo ilizinduliwa siku ya Jumatatu na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam au kama yanavyojulikana Saba Saba.

Dkt. Mwinyi alikuwa katika hafla ya ufunguzi rasmi ya maonesho hayo ya 49 katika uwanja wa maonesho wa Mwalimu Julius K. Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Akizunguma katika hafla hiyo. Dkt. Mwinyi alisema nembo hiyo itakuwa chachu ya kukuza uzalendo wa kibiashara na kuhimiza raia wa Tanzania kununua bidhaa zinazotengenezwa nchini humo.

Maonesho hayo yanafanyika kuanzia tarehe 28 Juni hadi 13 Julai.

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us