Iran imerusha makombora kadhaa Israeli katika kile inachoonekana kuzidisha makabiliano, huku vyombo vya habari vya Iran vikitangaza kuwa yamelenga moja kwa moja Tel Aviv, na moto kuwaka katika kambi kadhaa za karibu za kijeshi, ikiwemo Makao Makuu ya Wizara ya Ulinzi, kulingana na vyombo vya habari vya Israeli.
Mashambulizi haya ambayo hayakutarajiwa Ijumaa jioni, yaliyothibitishwa na chombo cha habari cha serikali cha Iran na kikosi cha jeshi cha IRGC, yamedhihirisha mashambulizi ya moja kwa moja ya Iran ya kijeshi kwa Israeli.
Televisheni ya taifa ya Iran ya Press TV imesema "awamu ya kwanza" ya mashambulizi ya makombora yalikuwa na "athari ya moja kwa moja" mjini Tel Aviv, huku chombo cha habari cha Israeli Channel 13 kikithibitisha kushindwa kuzuiliwa kwa makombora hayo, kufanya makombora kadhaa kulenga maeneo mbalimbali kote nchini.
Mwandishi wa habari wa shirikal la AFP mjini Tel Aviv alieleza kuwepo kwa moshi sehemu kubwa ya mji huo huku mashambulizi yakirindima usiku. Kumekuwepo na taarifa za moto karibu na majengo ya serikali na maeneo ya usalama, na maafisa wa dharura wakijaribu kukabiliana na hali hiyo.
Jeshi la IRGC limetoa taarifa likisema "limefanya mashambulizi dhidi ya maeneo kadhaa nchini Israeli", huku afisa mmoja mwandamizi wa Iran akiliambia shirika la habari la Reuters: "Hakuna mahali patakuwa salama nchini Israeli, kulipiza kwetu kisasi kutakuwa kwa njia ya uchungu."
Jeshi la Israeli limekiri kusikika kwa milipuko kote nchini lakini likasema ni matokeo ya kuzuiliwa kwa makombora na baadhi ya makombora kufanikiwa kulenga maeneo. Hakukuwa na taarifa zaidi za haraka kuhusu watu wangapi wamefariki au hasara iliyofanyika.
Mashambulizi haya yanajiri saa kadhaa baada ya Kiongozi wa Kidini wa Iran Ali Khamenei kuapa "kuwakabili vikali" kwa njia ya kisasi kwa kile alichokitaja kuwa Israeli kutangaza vita..
"Israeli imeanzisha hivi vita. Tutalipiza kisasi vibaya sana," Khamenei alisema kupitia hotuba iliyokuwa imerekodiwa awali.
Mashambulizi haya yanakuja baada ya Israeli kushambulia Iran mapema Ijumaa asubuhi, wakilenga kile Israeli ilichosema miundombinu ya nyuklia.