Kwa Picha : Tamasha la kitamaduni la vinyago huko Porto Novo, Benin, linaonyesha vinyago vya kipekee
Kwa Picha : Tamasha la kitamaduni la vinyago huko Porto Novo, Benin, linaonyesha vinyago vya kipekee
Duru ya pili ya Tamasha la Kitamaduni la vinyago limefanyika nchini Benin.
3 Agosti 2025

Tamasha la kitamaduni la vinyago huko Porto Novo, Benin, linaonyesha vinyago vya kipekee vya nchi na mavazi ya mwili mzima, ambayo yanafungamana na mila na desturi za kale.

Tamasha hili ambalo ni la pili kufanyika, lina mada "Ifá Orúnmìlà: Utangulizi wa elimu ya ufahamu wa imani ya kale na historia ya utamaduni." imehudhuriwa na watafiti, wasomi, wataalamu, na wakereketwa kutoka kote ulimwenguni kushiriki katika mazungumzo ya kina kuhusu mifumo ya maarifa asilia ya Kiafrika.

Maelfu ya watu walijitokeza kwa mavazi na kucheza densi za kitamaduni wakati wa tamasha hili la vinyago.

CHANZO:AP
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us