UTURUKI
1 dk kusoma
Rais wa Uturuki Erdogan ampongeza Starmer kwa msimamo wake wa dola ya Palestina
Katika mazungumzo yake na simu, Recep Tayyip Erdogan amesisitiza umuhimu wa kuchukua hatua za kuishinikiza Israel kusitisha mashambulizi na kulipa kipaumbele suluhu ya dola mbili.
Rais wa Uturuki Erdogan ampongeza Starmer kwa msimamo wake wa dola ya Palestina
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan./Picha:Reuters
4 Agosti 2025

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amempongeza Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer kwa kauli zake kuitambua dola ya Palestina.

 Katika mazungumzo yao ya simu siku ya Jumatatu, viongozi hao walijadiliana uhusiano kati ya Uturuki na Uingereza, pamoja na masuala mengine yakiwemo ya kikanda na kiulimwengu, ilisema Kurugenzi ya Mawasiliano ya Uturuki.

Kulingana na Erdogan, hali ya kibinadamu huko Gaza imefikia hatua mbaya na kwamba kunahitajika jukumu la kibinadamu kutatua tatizo hilo na sio kutoa sauti za masikitiko tu.

Pia, alisisitizia umuhimu wa kuishinikiza Israel kusitisha mashambulizi na kulipa kipaumbele suluhu ya dola mbili.

Erdogan aliongeza kuwa Uturuki inaendelea kupeleka misaada ya kibinadamu huko Gaza, ikiunga mkono jitihada za kusitisha mapigano na usuluhishi.

 

CHANZO:AA
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us