MICHEZO
2 dk kusoma
Marefa wanawake CHAN 2024
Katika mashindano ya CHAN 2024 kuna jumla ya waamuzi 70 walioteuliwa wakiwa wanatoka katika mataifa 30.
Marefa wanawake CHAN 2024
Waamuzi wanawake. / X @Fimboo0
4 Agosti 2025

Kuna waamuzi wa kati, wale wasaidizi na wale wa Video ya Kumsaidia Refa (VAR).

Miongoni mwao kuna marefa wanawake wakiwemo waamuzi wa kati Shamirah Nabadda kutoka Uganda na Bouchra Karboubi wa Morocco.

 Marefa wasaidizi ni Diana Chikotesha kutoka Zambia na Atezambong Fomo Carine wa Cameroon.

 Shamirah wa Uganda ndiye aliyekuwa Pilato wa mchezo wa Jumapili kati ya Madagascar na Mauritania, mechi ya kundi B ambapo matokeo yalikuwa sare ya sifuri kwa sifuri.

 Anafahamika kwa kuwa mwamuzi katika Olimpiki za mwaka 2024. Amewahi kuwa refa wa mashindano ya wanawake 2022 na 2023.

 Amekuwa mwamuzi mdogo mwanamke wa kati katika ligi kuu ya Uganda kipindi hicho akiwa na miaka 23.

Shamirah ambaye ni mzaliwa wa mji wa Mbarara, magharibi mwa Uganda ana umri wa miaka 30.


Bouchra Karboubi wa Morocco ana miaka 38 na refa mzoefu. Alianza kuchezesha mechi za barani Afrika 2018.

2020 akawa mwanamke wa kwanza kushika kipyenga katika ligi kuu ya wanaume nchini Morocco.

 Januari 2024 akawa mwanamke wa kwanza kutoka Afrika Kaskazini na mataifa ya kiarabu kuwa mwamuzi wa mechi ya wanaume ya AFCON 2023 Guinea Bissau dhidi ya Nigeria.

Olimpiki ya 2024 Paris alichezesha mechi kati ya Hispania na Japan.

Hatua hii huenda ikachagiza wanawake wengi zaidi kutoka barani Afrika kujitokeza kwa lengo la kupata fursa ya kuchezesha mechi zaidi za ngazi ya kimataifa.

CHANZO:TRT Afrika Swahili
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us