AFRIKA
3 dk kusoma
Ghana inatakiwa kuachana na mkakati wa ilani na kuwa na mtazamo wa kimaendeleo
Mikakati ya kimaendeleo yenye mifumo ya mipango na utekelezaji kulingana na raslimali zilizopo, ikiwemo vifaa, watu na muda.
Ghana inatakiwa kuachana na mkakati wa ilani na kuwa na mtazamo wa kimaendeleo
John Dramani Mahama alirejea uongozini kama rais wa 14 wa Ghana baada ya uchaguzi mkuu 2024 / AFP
4 Agosti 2025

Utegemezi wa Ghana katika mkakati wa ilani kwenye suala la maendeleo ni changamoto kubwa katika kuendeleza nchi kwa ujumla.

Kila inapofika wakati wa uchaguzi mkuu, vyama vya kisiasa na wagombea wao wa urais wanawapa majukumu wanachama kuandaa ilani, ambayo inakuwa kaulimbiu ya kampeni za chama na dira kwa taifa.

Vyama vya kisiasa hutegemea ilani zao kama mkakati wa maendeleo ya nchi ya Ghana, na kama itakayowaokoa kutoka kwa changamoto nyingi.

Hata hivyo, historia imeonesha kuwa ilani haitafsiriki kuwa maendeleo endelevu.

Ushahidi unadhihirika katika miradi mingi ambayo haijakamilika kote nchini Ghana.

Miradi hii inaanzishwa, lakini haikamiliku. Hii ni kwa sababu, kwa njia moja au nyingine, iliahidiiwa katika ilani za vyama bila kuangalia kama kuna raslimali za kutosha za kukamilisha miradi hiyo, ikiwemo muda wa kukamilisha.

Dira ya Nkrumah

Hata hivyo, katika nia yao ya kuwa na maendeleo endelevu, pamoja na raslimali zetu chache, ni muhimu katika kupunguza uharibifu, na kukakikisha matumizi mazuri ya raslimali za Ghana.

Mikakati ya kufanya maendeleo ni bora sana kuliko kutegemea mfumo ulioko sasa wa ilani.

Inatambua nchi ilipo kwa sasa na raslimali zinazohitajika katika kutekeleza matatizo ya kiuchumi na kijamii wakati mipango ya maendeleo ya nchi yakizingatiwa.

Tangu uhuru, kumekuwa na juhudi za kuchagiza mtazamo huo wa maendeleo nchini Ghana, huku Rais wa kwanza Kwame Nkrumah akiweka mkakati wa kuigwa.

Historia inaonesha kuwa Nkrumah aliweka msingi thabiti (kwa mfano., barabara, viwanda vya ndani, umeme na kadhalika.) ambao umesaidia kuimarisha ukuaji na maendeleo nchini Ghana.

Leo, usambazaji wa umeme nchini Ghana unategemea zaidi utashi wa Nkrumah. Hata hivyo, mipango mingi ya maendeleo ya Nkrumah hayangeweza kuendelezwa kutokana na kubadilishwa kwa serikali mara kwa mara.

Utumiaji mzuri wa raslimali

Hata hivyo, kutegemea zaidi ilani za vyama vya kisiasa kwa maendeleo ya Ghana kumedunisha jukumu muhimu na umuhimu wa Tume ya kuratibu maendeleo NDPC nchini Ghana.

Kutokana na kujaribu maendeleo yanayotegemea ilani kwa miongo miwili au mitatu bila kuwa na matokeo mazuri kwa maendeleo ya Ghana, ni wakati sasa wa kufikiria kuhusu mipango ya msingi ya maendeleo.

Kuwa na mfumo wa maendeleo ambao umejumuishwa katika katiba.

Hili litafanya kukubaliwa kwa mpango huo wa maendeleo. Ni muhimu pia kwa mpango wa Ghana kuwa na agenda mahsusi ambayo itaangalia kwa makini mahitaji ya nchi ya sasa na ya baadaye.

Kwa mfano, huku ikuwa mpango wa miaka 5 unatumika kote duniani, Ghana inaweza kuwa na mpango wake wa miaka 4 ambao unaenda sanjari na muda wa muhula wa serikali, kwa hiyo kupunguza matatizo ya kutoendelea kwa miradi pale panapokuwa na mabadiliko ya serikali.

Ghana haiwezi kukaa na kutegemea mafanikio yake ya zamani lakini inatakiwa kuwa na mipango endelevu ya maendeleo kwa nchi hiyo.

Huku mataifa yakiendelea kupata maendeleo endelevu, ni muda sasa wa kutafakari upya na kuondosha mfumo wa kutegemea ilani, kwa lengo la kupata maendeleo yenye tija Ghana.

Mwandishi, Dkt. Peter Asare-Nuamah ni mhadhiri katika Chuo cha Mazingira na Maendeleo Endelevu, Ghana, na Mtafiti Mwandamizi katika Kituo cha Utafiti wa Maendeleo,Chuo Kikuu cha Bonn, Ujerumani.

Kanusho: Maoni ya mwandishi hayaakisi maoni, mitazamo na sera za uhariri za TRT Afrika.

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us