ULIMWENGU
2 dk kusoma
Uhusiano na China 'umepiga hatua': Waziri Mkuu wa India
Safari ya Wang nchini India baada ya uhusiano kati ya majirani hao wawili kudhoofika 2019, na kusababisha mapigano mpakani mwa kanda ya Ladakh katika eneo linalosimamiwa na India la Jammu na Kashmir mwezi Mei 2020.
Uhusiano na China 'umepiga hatua': Waziri Mkuu wa India
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi anasema uhusiano na China ‘’umepiga hatua kubwa.’’ / AP
20 Agosti 2025

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi amesema siku ya Jumanne kuwa uhusiano wao na China “umepiga hatua ”.

Alitoa matamshi hayo baada ya ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi ambaye alipokelewa na waziri mkuu wa India jijini New Delhi.

“Nimefurahi kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje Wang Yi,” Modi aliandika kwenye mtandao wa kijamii wa kampuni ya Marekani wa X.

Kuimarika huku kwa uhusiano kumeongozwa na “heshima miongoni mwetu na maslahi,” amesema Modi, akitoa wito wa ‘‘uthabiti, utekelezaji, na uhusiano wenye tija,” ambao utachangia pakubwa katika kanda pamoja na “amani duniani na mafanikio.”

Mapema siku ya Jumanne, mwanadiplomasia huyo wa China alikutana na mshauri wa usalama wa taifa wa India Ajit Doval kwa hatua ya 24 ya mazungumzo kuhusu mpaka.

Safari hii inakuja huku uhusiano wa kimkakati wa Marekani na India ukiwa umeteteleka katika muhula wa pili wa Rais wa Marekani Donald Trump, wakati Marekani ikiiadhibu India kwa kuiwekea ushuru wa asilimia 50, kwa kushtumu nchi hiyo yenye idadi kubwa ya watu duniani kwa kutofanya “biashara vizuri” na “kufadhili” Urusi wakati mapigano yanaendelea Ukraine.

Maafisa wa India wanasema Wang alikuwa na ujumbe na mualiko kutoka kwa Rais wa China Xi Jinping kwa Modi kwa lengo la viongozi hao kuwa na mkutano wa Ushirikiano wa Shanghai huko Tianjin baadaye mwezi huu.

Modi alimshkuru Xi kwa mualiko huo na kueleza kukubali kwake, alisema katika taarifa ya India. Aliongeza kuwa Modi "alisisitiza kuhusu uthabiti, na uhusiano wenye tija kati ya India na China utachangia pakubwa katika amani ya kanda na dunia pamoja na mafanikio.”

Pande mbili kuunda kundi la wataalamu kuhusu masuala ya mpakani

Wang alimwambia Doval kuwa uhusiano “umeingia katika hatua muhimu ya maendeleo,” huku suala la mpaka likiendelea “kuwa salama na kuimarika,” kulingana na taarifa ya China.

Amesema kuwa mataifa hayo mawili “yana maoni na maslahi ya pamoja,” akiwaomba “kuendeleza kuaminiana kupitia majadiliano na mawasiliano, kubadilishana mawazo na ushirikiano … kwa kuimarisha na kuendeleza uhusiano wa mataifa mawili.”

Wizara ya Mambo ya Nje ya India inasema pande zote mbili zimekubaliana kuanzisha kundi la wataalamu “kuangalia suala la mpaka” pamoja na kuunda kundi “litakaloandaa mkakati wa usimamizi mzuri wa mpakani kuhakikisha amani na utulivu,” katika eneo hilo la mpakani.

CHANZO:AA
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us