AFRIKA
1 dk kusoma
Jamhuri ya Afrika ya Kati kufanya uchaguzi mkuu Disemba 28
Wapigaji kura milioni 2.3 wamejisajili kwa ajili ya uchaguzi wa urais, ubunge, serikali za mitaa, na uchaguzi wa manispaa, kulingana na afisa
Jamhuri ya Afrika ya Kati kufanya uchaguzi mkuu Disemba 28
tokea masaa 7

Jamhuri ya Afrika ya Kati itafanya uchaguzi wake mkuu Disemba 28, baada ya kuahirishwa mara kadhaa, afisa wa serikali alithibitisha siku ya Jumanne.

Wapiga kura watashiriki katika uchaguzi wa urais, ubunge, serikali za mitaa na manispaa, Bruno Yapande, waziri aliwaambia waandishi wa habari, kufuatia mkutano na tume ya uchaguzi, ambayo na jukumu la kuweka sawa daftari la wapiga kura.

Mchakato wa uchaguzi unaendelea vizuri, licha ya kuwepo na changamoto, alisema.

Watu karibu milioni 2.3 wamejisajili kwa uchaguzi huo, na orodha ya mwisho inatarajiwa kuwa tayari Agosti 29, waziri huyo alisema.

Rais Faustin Archange Touadera, ambaye alichaguliwa kwa mara ya kwanza 2016 na kuchaguliwa tena 2020, ametangaza nia yake mwezi Julai ya kuomba muhula wa tatu huku kukiwa na upinzani kuhusu hatua hiyo.

Anasifika kwa kuimarisha hali ya usalama baada ya miaka ya kuwa kwenye mapigano.

CHANZO:TRT Afrika Swahili
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us