AFRIKA
2 dk kusoma
Somalia inakabiliwa na ongezeko la dondakoo kutokana na uhaba wa chanjo na kupungua misaada
Dondakoo au Diphtheria, ugonjwa wa bakteria unaosababisha kuvimba kwa tezi, matatizo ya kupumua na homa na huathiri zaidi watoto, unaweza kuzuilika kwa chanjo iliyopatikana kwa wingi katikati ya karne ya 20.
Somalia inakabiliwa na ongezeko la dondakoo kutokana na uhaba wa chanjo na kupungua misaada
Bajeti kubwa ya Afya ya somalia inategemea ufadhili wa nje / Reuters
tokea masaa 5

Maambukizi ya ugonjwa wa Dondoakoo au Diphtheria yameongezeka kwa kasi mwaka huu nchini Somalia, ambapo matibabu yameathiriwa na uhaba wa chanjo na kupunguzwa kwa misaada ya Marekani, maafisa wa Somalia walisema.

Zaidi ya maambukizi 1,600, ikiwa ni pamoja na vifo 87, zimerekodiwa, kutoka kesi 838 na vifo 56 katika mwaka wote wa 2024, alisema Hussein Abdukar Muhidin, mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Kitaifa ya Afya ya Somalia.

Dondakoo au Diphtheria, ugonjwa wa bakteria unaosababisha kuvimba kwa tezi, matatizo ya kupumua na homa na huathiri zaidi watoto, unaweza kuzuilika kwa chanjo iliyopatikana kwa wingi katikati ya karne ya 20.

Viwango vya chanjo ya watoto nchini Somalia vimeimarika katika muongo mmoja uliopita, lakini mamia ya maelfu ya watoto bado hawajachanjwa kikamilifu.

Bajeti kubwa ya afya inategemea wafadhili

Waziri wa Afya Ali Haji Adam alisema serikali ilijitahidi kupata chanjo ya kutosha kutokana na uhaba wa kimataifa na kwamba kupunguzwa kwa misaada ya Marekani kunafanya iwe vigumu kusambaza dozi ilizokuwa nazo.

Kabla ya Rais Donald Trump kukata misaada mingi ya kigeni mapema mwaka huu, Marekani ilikuwa mfadhili mkuu wa kibinadamu kwa Somalia, ambayo karibu bajeti yake ya afya yote inafadhiliwa na wafadhili.

"Kukatwa kwa misaada ya Marekani kuliathiri sana fedha za afya ilizokuwa zikitoa kwa Somalia. Vituo vingi vya afya vilifungwa. Timu za chanjo zinazohamishika ambazo zilipeleka chanjo katika maeneo ya mbali zilipoteza ufadhili na sasa hazifanyi kazi," alisema Adam.

Ahadi za jumla za usaidizi wa kigeni wa Marekani kwa Somalia zinafikia dola milioni 149 kwa mwaka wa fedha unaomalizika Septemba 30, ikilinganishwa na dola milioni 765 katika mwaka wa fedha uliopita, kulingana na takwimu za serikali ya Marekani.



CHANZO:Reuters
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us