UTURUKI
1 dk kusoma
Mke wa Rais wa Uturuki Emine Erdogan aingia rasmi mtandao wa kijamii wa Uturuki wa NEXT Sosyal
Kufikia Agosti 16, jukwaa la NEXT Sosyal lilikuwa limepita idadi ya watumiaji milioni 1, huku likiendelea.
Mke wa Rais wa Uturuki Emine Erdogan aingia rasmi mtandao wa kijamii wa Uturuki wa NEXT Sosyal
Mke wa Erdogan achapisho kwenye mtandao wa NEXT Sosyal./Picha: AA
19 Agosti 2025

Mke wa rais wa Uturuki Emine Erdogan atumia mtandao wa kijamii wa Uturuki wa NSosyal kwa mara ya kwanza, kwa ujumbe wa furaha na shukrani.

"Habari kutoka NSosyal. Nina furaha ya kuwa sehemu ya mtandao huu wa kijamii ulio huru na asilia, natoa shukrani zangu za dhati kwa kila mtu anayetupa fahari kama taifa," alisema kupitia chapisho lake siku ya Jumanne.

InayohusianaEmine Erdoğan (@emineerdogan@sosyal.teknofest.app)

"Katika ulimwengu huu salama wa kidijitali, tutafikiri na kuzalisha kile chenye kutupa tunu zetu. Tuko tayari kwa safari mpya tukiwa na NSosyal."

Kuingia kwake kwenye mtandao huo kunakuja siku moja baada ya Rais Recep Tayyip Erdogan ajisajili kwenye mtandao wa NSosyal.

Mtandao wa NSosyal umetengenezwa kupitia uongozi wa Timu ya Teknolojia ya Uturuki (T3), na ulivuka idadi ya watumiaji milioni 1 kufikia Agosti 16, huku ukiendelea kukua kwa kasi.

Likichagizwa kuwa kama jukwaa “safi na salama” limeibuka kama moja ya mitandao maarufu ya kijamii kwa sasa.

Toka kuanzishwa kwake, jukwaa hilo limezidi kukua, likitoa fursa kwa watumiaji wake kutoa maoni yao kuhusu masuala mbalimbali ya kimaisha.

Hatua ya Rais wa Uturuki na mke wake kujisajili katika mtandao huo, ni ishara ya kulipa jukwaa hilo nguvu na umaarufu pamoja na kukuza jitihada ya Uturuki ya kuendeleza majukwaa ya kidijitali.

CHANZO:AA
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us