UTURUKI
2 dk kusoma
Ziara ya Erdogan Somalia 2011 ilikuwa ya mabadiliko kwa historia ya nchi: waziri wa Somalia
Ziara ya Rais Recep Tayyip Erdogan ya kihistoria nchini Somalia 2011, wakati akiwa waziri mkuu, iliacha athari kubwa kwa kumbukumbu za watu.
Ziara ya Erdogan Somalia 2011 ilikuwa ya mabadiliko kwa historia ya nchi: waziri wa Somalia
Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Somalia anasema ziara ya Erdogan 2011 iliangazia misaada, huku ziara yake ya 2016 ikawa ya maendeleo. / AA Maktaba
20 Agosti 2025

Ziara ya Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan nchini Somalia 2011 ilikuwa ya kihistoria na kubadilisha hatma ya nchi hiyo, waziri wa Somalia amesema.

Waziri wa Bandari na Uchukuzi wa Somalia Abdulkadir Mohamed Nur ameliambia shirika la habari la Anadolu katika mahojiano kuwa ziara ya Erdogan Agosti 2011 ilifanyika wakati wa kipindi kigumu zaidi kwa Somalia tangu mifumo ya taifa hilo kuporomoka mwaka 1990.

Ziara ya Erdogan mjini Mogadishu na mkewe Emine Erdogan, watoto, na mawaziri inakumbukwa kama siku ambayo haitosahauliwa Somalia, ambayo wakati huo ilikuwa inapitia kipindi kibaya cha ukame katika historia ya nchi hiyo, Nur alisema.

Baadhi ya maafisa wa Somalia wanasema ziara hii ilibadilisha muelekeo wa nchi hiyo na kuiondoa nchi katika kutengwa na kulifanya iwe katika agenda ya kimataifa, na kuimarisha uhusiano wa Uturuki na Somalia hadi katika ngazi ya kimkakati.

Nur alieleza kuwa Somalia, ambayo ilionekana kutengwa tangu mifumo ya serikali kuporomoka 1990, ilipitia kipindi kigumu cha ukame katika historia ya nchi hiyo.

"Siku hizo, Somalia ilikuwa nchi ambayo imetengwa na dunia na bila msaada. Wakati Rais Erdogan, pamoja na baraza lake, familia, na maafisa wake wote, alipowasili Somalia, mabadiliko makubwa yalitokea. Siyo tu kwa Uturuki kupokea misaada, lakini dunia nzima ilianza kuangazia Somalia," alieleza.

Nur alisisitiza kuwa Uturuki haijawahi kuitenga Somalia tangu wakati wa ziara ya Erdogan, akisema, "Tangu wakati huo, tumeimarika kila siku. Mchango wa Uturuki kwa ujenzi upya wa Somalia umekuwa wa muhimu sana."

Nur alieleza kuwa Uturuki muda wote imekuwa ikiunga Somalia mkono katika vita vyake dhidi ya ugaidi, maendeleo yake, na mafanikio ya watu wake.

Mohamed Dhuubow, Mkurugenzi wa Ofisi ya Uwekezaji ya Somalia katika Wizara ya Mipango, Uwekezaji na Maendeleo ya Kiuchumi, alizungumzia kuhusu ziara za Erdogan, akisema, "Ziara ya 2011 ilikuwa kwa ajili ya misaada kwa watu, lakini ziara ya pili 2016 ilikuwa ya maendeleo."

Dhuubow alisema kuwa jukumu la Uturuki nchini Somalia limehama na liko katika uwekezaji na miundombinu.

Kufunguliwa kwa ubalozi mjini Mogadishu, kuanzishwa kwa Ofisi ya Uturuki ya Ushirikiano na Uratibu (TIKA), na kufunguliwa kwa shule za Uturuki na Hospitali yote yameimarisha uhusiano kitaasisi.

Leo, Somalia imekuwa alama ya Uturuki katika kuimarisha Afrika. Makampuni ya Uturuki yanadhihirika katika ujenzi wa miundombinu ya Somalia na katika maisha ya kila siku ya watu, huku nchi hizi mbili zikiangazia ushirikiano katika sekta ya nishati, uvuvi, na hata masuala ya anga.

CHANZO:AA
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us