AFRIKA
2 dk kusoma
Uturuki yaongeza juhudi za kupatikana kwa 'Libya yenye umoja'
Uturuki inaunga mkono juhudi za majadiliano nchini Libya zenye lengo la kuimarisha umoja wa taifa hilo na uhuru wake.
Uturuki yaongeza juhudi za kupatikana kwa 'Libya yenye umoja'
Meli ya jeshi la wanamaji la Uturuki TCG Kinaliada ilikuwa katika bandari ya Tripoli mapema wiki hii. / Wengine
20 Agosti 2025

Uturuki inaendeleza juhudi za kidiplomasia zenye lengo la kumaliza mapigano nchini Libya na kuwa na "Libya yenye umoja", kulingana na vyanzo vya wizara ya Ulinzi ya Uturuki

Msukumo huo umeanza kwa ziara ya Mkuu wa Majeshi ya Nchi Kavu wa Libya, Luteni Jenerali Saddam Haftar, Uturuki Aprili 2025. 

Mapema wiki hii, meli ya jeshi la wanamaji ya Uturuki TCG Kınalıada ilifanya ziara katika bandari ya Tripoli ambapo kulikuwa na mkutano kati ya Balozi wa Uturuki nchini Libya, Güven Begeç, na waziri wa ulinzi wa Libya, mkuu wa majeshi, kamanda wa jeshi la wanamaji, kamanda wa ulinzi wa maeneo ya bahari na kamanda wa Tripoli.

TCG Kınalıada inatarajiwa kufanya ziara bandari ya Benghazi siku ya Jumatano, wakati ambapo kutakuwa na ziara ya kijeshi na makaribisho rasmi kwenye meli hiyo. 

Mtazamo wa kuleta uthabiti

Ziara hiyo inadhihirisha mtazamo wa Uturuki wa kujumuisha watu wote nchini Libya na sera yake inayoendelea yenye lengo la kujumuisha nchi nzima. 

TCG Kınalıada ilifanya ziara katika bandari ya Tripoli, Libya, mapema wiki hii. Baada ya kuondoka Bandari ya Tripoli, itafanya mazoezi baharini pamoja na boti ya mashambulizi ya Shafak ya jeshi la Wanamaji la Libya. 

Mwezi Aprili 2025, Luteni Jenerali Saddam Khalifa Hafter, Kamanda wa Jeshi la Nchi Kavu, walitembelea Uturuki na walipokelewa jijini Ankara na Waziri wa Ulinzi wa Uturuki Yaşar Güler na Kamanda wa majeshi ya Nchi Kavu, ambaye sasa ni Mkuu wa Majeshi Jenerali Selçuk Bayraktaroğlu.

“Uturuki na Libya ni mataifa rafiki yenye uhusiano wa kihistoria na kitamaduni. Kuanzia mwanzo, lengo letu limekuwa kwa watu wa Libya kuishi kwa umoja, ushirikiano, amani na uthabiti,” vilisema vyanzo vya wizara ya ulinzi vya Uturuki kuhusu ziara hiyo.


CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us