20 Agosti 2025
Chama Cha Mapinduzi (CCM) cha nchini Tanzania, kitafanya kikao cha siku mbili chenye lengo la kufanya teuzi za Wagombea Ubunge, wa Bunge la nchi hiyo, wabunge wa Viti Maalumu, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Viti Maalum.
Kulingana na taarifa iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, anayeshughulikia itikadi, uenezi na mafunzo Amos Makalla, vikao hivyo ambavyo vitaongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM, vitafanyika Agosti 21 na 23, 2025 jijini Dodoma.
CHANZO:TRT Afrika Swahili