AFRIKA
1 dk kusoma
Raia wa Afrika kutolipia viza kuingia Burkina Faso
Hata hivyo, urahisi huo unaweza kubadilika baada ya nchi hiyo kujiondoa kutoka Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS).
Raia wa Afrika kutolipia viza kuingia Burkina Faso
Kiongozi wa kijeshi wa Burkina Faso, Kapteni Ibrahim Traoré./Picha:Wengine
tokea masaa 12

Raia wa Afrika wanaotarajia kuitembelea Burkina Faso, sasa hawatohitaji kulipia gharama za viza.

Hatua hiyo inalenga kukuza muingiliano wa watu na bidhaa ndani ya nchi hiyo, kulingana na Waziri wa Usalama wa Burkina Faso, Mahamadou Sana.

"Kuanzia sasa, raia atokaye nchi yoyote ya Kiafrika, hatolazimika kulipia gharama za viza ili aingie Burkina Faso,” alisema Sana, katika kikao cha baraza la mawaziri kilichoongozwa na Kapteni Ibrahim Traoré siku ya Alhamisi.

Hata hivyo, raia wa Kiafrika wanaotaka kuingia Burkina Faso, watahitajika kufanya maombi ya viza kwa njia ya mtandao kwanza kwa ajili ya kuhakikiwa.

Burkina Faso inaungana na nchi zingine kama vile Ghana, Rwanda na Kenya, ambazi zimerahisisha usafiri kwa raia wa Afrika.

Kwa sasa, raia wa kutoka nchi za Afrika Magharibi wanaruhusiwa kuingia Burkina Faso bila Viza.

CHANZO:TRT Afrika Swahili
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us