Vichwa vya nguruwe vimeoneka katika misikiti kadhaa mjini Paris, mamlaka zimesema, wakilaani matusi hayo kwa jamii ya Kiislamu.
Polisi nchini Ufaransa imeanzisha uchunguzi Jumanne baada ya vichwa vya nguruwe kuonekana nje ya misikiti kadhaa katika mji wa Paris, amesema mkuu wa polisi wa eneo hilo.
“Kila jitihada zinafanywa ili kuwakamata wahusika wa vitendo hivyo vibaya,” Laurent Nunez ameandika katika X.
Vichwa hivyo vimeonekana katika barabara mjini Paris na maeneo matatu ya jirani, kwa mujibu wa mamlaka za eneo hilo.
Waziri wa Mambo ya Ndani Bruno Retailleua amelaani vitendo hivyo, akiviita “za ajabu” na “visivyokubalika.”
“Nataka mwenzetu wa dini ya Kiislamu kufanya ibada yao kwa amani,” amesema.
‘Kuongezeka kwa chuki dhidi ya Waislamu ’Chems-Eddine Hafiz, mkuu wa Msikiti Mkuu wa Paris, ameshutumu vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu na kusema ni vimefikia kiwango kipya na hatari, huku akitaka kutolewe elimu na kuwepo kwa mshikamano wa kitaifa.
Ufaransa ina idadi kubwa ya Waislamu, zaidi ya milioni 6, ambao kwao nguruwe ni najisi.
Nchi kadhaa za ulaya imeripoti ongezeko la “chuki dhidi ya Waislamu” tangu kuanza kwa vita vya Gaza Oktoba 2023, kwa mujibu wa Wakala wa Haki za Msingi wa Umoja wa Ulaya.
Israel inafanya mauaji ya halaiki Gaza, ambapo wameua zaidi ya Wapalestina 64,000 tangu Oktoba 7, 2023.
Ukatili wa Israel unaendelea huku Waziri Netanyahu akitoa vitisho vya mashambulizi zaidi kwa Palestina iliyozingirwa.