Viongozi wa Afrika, wasisitiza utelekezaji wa maazimio ya Mkutano wa Tabianchi uliofanyika Ethiopia
MAZINGIRA
2 dk kusoma
Viongozi wa Afrika, wasisitiza utelekezaji wa maazimio ya Mkutano wa Tabianchi uliofanyika EthiopiaViongoizi wa seriklai na wengine wa tabaka mbali mbali walikutana katika mkutano wa pili wa kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi uliofanyika jijini Addis Ababa nchini Ethiopia kuanzia Septemba 8 hadi 10, 2025.
Mkutano wa pili wa bara wa mabadiliko ya tabia nchi uliwaleta pamoja washikadau tofauti @ACS2ET / Public domain
tokea masaa 19

Bara la Afrika limesisitiza umuhimu wa kuwekeza zaidi katika suluhisho ya kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa.

“Azimio la viongozi lilitoa wito wa "kuimarishwa na kuungwa mkono juhudi endelevu ili kuongeza utekelezaji wa mipango ya hali ya hewa inayoongozwa na Afrika kama vile Mpango wa Ukuta wa Kijani Kibichi wa Umoja wa Afrika, Mpango wa Kurejesha Mazingira ya Misitu ya Afrika, na Mpango wa Urithi wa Kijani wa Ethiopia,” imesema sehemu ya azimio la Mkutano wa pili wa bara kuhusu tabianchi.

Mkutano huo uliofanyika jijini Addis Ababa nchini Ethiopia Septemba 8 hadi 10, 2025, ulihudhuriwa na marais William Ruto wa kenya, Salva Kiir wa Sudan Kusini, Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia, na Ismaïl Omar Guelleh wa Djibouti.

Viongozi wa Afrika walitoa ahadi za kifedha na ubunifu kwa ajili ya utekelezaji wa ufumbuzi unaoongozwa na Afrika.

Walivumbua mipango kama “Africa Climate Innovation Compact (ACIC) na African Climate Facility (ACF),” kwa ajili ya kuwekeza fedha za kupambana na majanga ya tabianchi.

“Waziri Mkuu wa Ethiopia alijitolea kukusanya dola bilioni 50 kila mwaka ili kuleta utatuzi wa changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa,” ilisema sehemu ya azimio la pamoja.

“Mkataba huo unalenga kutoa suluhu 1,000 za Kiafrika ili kukabiliana na changamoto za hali ya hewa katika nishati, kilimo, maji, usafiri na ustahimilivu ifikapo 2030,” iliongezea.

Viongozi waliweka wazi kwamba fedha za kukabiliana na hali hiyo ni wajibu wa kisheria kutoka kwa nchi zilizoendelea.

“Afŕika ilisisitiza kuwa fedha za kukabiliana na hali hiyo lazima ziwasilishwe kwa njia ya ruzuku, na siyo mikopo ambayo inazidisha mzigo wa madeni,” taarifa ya pamoja ya mkutano huo wa pili wa kibara ilisema.

“Ili kurekebisha hali ya kukosekana kwa usawa wa kifedha wa hali ya hewa barani Afrika, makubaliano ya kihistoria yalifanywa ili kutekeleza Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi wa Afrika uliosubiriwa kwa muda mrefu, unaoungwa mkono na Benki ya Maendeleo ya Afrika, ambao utapitisha dhamana za kijani na vyombo vya ufadhili vya ubunifu vilivyojengwa kwa hali halisi ya Afrika.”

Viongozi zaidi walitaka sehemu ya Afrika ya uwekezaji wa nishati safi kuongezeka kutoka asilimia 2 hadi angalau asilimia 20 ifikapo 2030, mabadiliko ambayo hatimaye yangeakisi uwezo wa bara kama nguvu ya nishati mbadala.

Mkutano huo ulisukuma Mkakati wa Madini ya Kijani, mpango wa kuhakikisha kwamba kobalti, lithiamu, shaba, na ardhi adimu huchochea sio tu minyororo ya usambazaji wa nishati safi duniani lakini pia manufaa ya ndani, uundaji wa nafasi za kazi, na uanzishaji wa viwanda.

CHANZO:TRT Swahili
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us