AFRIKA
1 dk kusoma
Hamas yakubali mapendekezo ya wapatanishi kusitisha mapigano siku 60 Gaza: Vyombo vya Misri
Kundi la wapiganaji la Palestina Hamas limekubali mapendekezo ya kusitisha mapigano Gaza kwa siku 60 yaliyowasilishwa na wapatanishi wa Misri na Qatar, Vyombo vya habari vya Misri viliripoti Jumatatu.
Hamas yakubali mapendekezo ya wapatanishi kusitisha mapigano siku 60 Gaza: Vyombo vya Misri
Kundi la wapiganaji wa Palestina Hamas linasemekana kuridhia mapendekezo ya Misri ya kusitisha mapigano kwa siku 60. / Picha: AP
18 Agosti 2025

Kundi la wapiganaji la Palestina Hamas limekubali pendekezo la kusitisha mapigano Gaza kwa siku 60 yaliyowasilisjwa na wapatanishi wa Misri na Qatar, vyombo vya habari vya Misri viliripoti Jumatatu.

Shirika la habari la serikali Al-Qahera News, likitaja vyanzo nchini Misri, linasema kuwa kuna mipango ya kutoa wito kwa vikosi vya Israel kwenda maeneo ya mpakani kusaidia kupitishwa kwa misaada inayoelekea Gaza.

Mapendekezo hayo yanajumuisha kusitishwa kwa muda kwa operesheni za kijeshi kwa miezi miwili, ambapo kipindi hicho kutakuwa na kubadilishana kwa wafungwa, kulingana na taarifa hiyo.

Makubaliano hayo yanazingatia kuachiliwa huru kwa mateka 10 wa Israel walio hai na kurudishwa kwa miili 18, wakibadilishana kwa idadi ambayo haijajulikana ya wafungwa wa Palestina.

Hatua katika kuelekea kwa kutafuta suluhu ya kudumu

Vyanzo hivyo vinasema Hamas inaona mpango huo kama ni mzuri wa kulinda watu wa Gaza kutokana na mapigano ya wanajeshi pamoja na uwezekano wa kutafuta suluhu ya kudumu ya kusitisha mapigano.

Hakujakuwa na taarifa ya haraka kutoka kwa Hamas au wapatanishi kuhusu taarifa hiyo.

CHANZO:AA
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us