AFRIKA
2 dk kusoma
DRC, waasi wa M23 washindwa kufikia makubaliano ya amani ya Doha
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na waasi wa M23 wameshindwa kufikia muafaka wa makubaliano ya amani ya Doha katika siku ya mwisho iliyowekwa wao kufanya hivyo.
DRC, waasi wa M23 washindwa kufikia makubaliano ya amani ya Doha
Waasi wa M23 wamedhibiti maeneo mengi mashariki mwa DRC tangu mwanzoni mwa 2025. / Picha: AA
18 Agosti 2025

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na waasi wa M23 wameshindwa kufikia makubaliano ya amani ya Doha katika siku ya mwisho ya kufanya hivyo, kuongeza wasiwasi kati ya makundi hayo mawili kuwa mazungumzo yanaweza kutatizwa na kurejesha nyumba hatua zilizopigwa za kumaliza mapigano.

Mapigano mashariki mwa DRC yameongezeka mwaka huu, huku kundi la M23 likianzisha mapigano na kuchukuwa udhibiti wa miji mikubwa miwili.

Chini ya juhudi za upatanishi ziloongozwa na Qatar, DRC na waasi hao walitia saini azimio la makubaliano Julai 19 ambapo waliapa kuanza mashauriano kabla ya Agosti 8 na kwa lengo la kufikia Agosti 18.

Waasi wa M23 walisema katika taarifa Jumapili kuwa utekelezaji wa azimio, ambapo unajumuisha kuwaachia huru wafungwa, kungesaidia kuendelea na hatua nyingine ya mazungumzo.

Makubaliano

Chanzo kimoja cha kiongozi mwandamizi wa waasi wa M23 siku ya Jumatatu kilisema kuwa watatuma ujumbe mdogo kwenda Qatar kwa mazungumzo katika siku chache zijazo.

"Ujumbe wetu utatilia nguvu umuhimu wa kutekeleza hatua hizi kabla kuendelea na mazungumzo zaidi, " chanzo hicho kilisema.

Chanzo cha serikali kimesema mamlaka zimepokea rasimu ya makubaliano kutoka kwa kundi la wapatanishi, na pande zote zinafanyia kazi maoni yaliyotolewa kabla wajumbe warudi tena Doha baadaye wiki hii.

Afisa mmoja wa Qatar ameliambia shirika la habari la Reuters Jumapili kuwa pamoja na kuwa wameshindwa kufikia muda wa mwisho uliowekwa wa makubaliano, pande zote mbili zilieleza utayari wao wa kuendelea na mazungumzo.

CHANZO:TRT Afrika Swahili
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us