AFRIKA
1 dk kusoma
Sudan yawabana mabingwa Senegal na kufanikiwa kumaliza wa kwanza kundi D
Sudan na Senegal wote wamefuzu kwa robo fainali za CHAN 2024 baada ya kumaliza sare ya bila kufungana katika uwanja wa Amaan huko Zanzibar Jumanne usiku.
Sudan yawabana mabingwa Senegal na kufanikiwa kumaliza wa kwanza kundi D
Mechi ya Sudan na Senegal. / Picha: CAF
tokea masaa 5

Matokeo hayo yameihakikishia Sudan kumaliza kileleni mwa kundi D kwa tofauti ya magoli, huku mabingwa Senegal wakifuzu kwa kumaliza nafasi ya pili.

Wakati huo huo, Nigeria imeifunga Congo 2-0 jijini Dar es Salaam, lakini juhudi hizo za Tai wa Kijani hazikuwasaidia kuwaondoa Sudan na Senegal kwenye nafasi zao.

Ilisemekana kuwa mechi ya maamuzi ya kundi D, na naam ilikuwa kama ilivyotarajiwa, hata bila magoli.

Sudan, ambayo inafunzwa na kocha raia wa Ghana Kwesi Appiah, ilikuwa imechangamka sana baada ya kuicharaza Nigeria 4-0.

Senegal, mabingwa wa sasa, walifahamu kuwa iwapo wangeshindwa ina maana wangeyaaga mashindano lakini pia walikuwa na nia ya kumaliza wa kwanza kwenye kundi hilo,ambalo hilo halikutimia.

CHANZO:TRT Afrika Swahili
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us