28 Machi 2023
Umoja wa Afrika unaziomba pande zinazovutana nchini Kenya kushiriki katika mazungumzo ili kutatua tofauti zozote zinazoweza kuwepo.
Kauli ya Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahammat, inafuatia mvutano nchini humo huku viongozi wa upinzani wakishinikiza maandamano ya kila wiki kupinga gharama kubwa ya maisha.
Zilizopendekezwa
Huu ni wiki ya pili tangu maandamano kuanza. Baadhi ya watu wamepoteza maisha huku mali zikiharibiwa. Baadhi ya shughuli za Kiuchumi katika maeneo ya nchi zimetatizika wakati wa maandamano hayo.
AU inasema itaunga mkono juhudi za Serikali na Wananchi wa Kenya katika kuleta umoja wa kitaifa, amani na utulivu nchini.
CHANZO:TRT Afrika