ULIMWENGU
1 DK KUSOMA
Urusi yatwaa Urais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa  'pigo'  kwa Kiev
Mzozo wa Urusi na Ukraine sasa uko katika siku yake ya 402. Huku Urusi ikitwaa moja ya viti muhimu katika umoja wa mataifa.
Urusi yatwaa Urais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa  'pigo'  kwa Kiev
UN Security Council / Photo: Reuters
1 Aprili 2023

Afisa wa ngazi ya juu wa Ukraine amekosoa 'ishara ya pigo' kwa Urusi kutwaa urais wa zamu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

"Siyo aibu tu. Ni pigo jingine la kiishara kwa mfumo unao zingatia sheria za uhusiano wa kimataifa," Andriy Yermak, mkuu wa wafanyakazi wa rais wa Ukraine, aliandika kwa Kiingereza kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Siku ya Jumamosi Urusi imechukua nafasi ya urais wa baraza kuu la usalama la Umoja wa Mataifa, ambalo huzunguka kila mwezi.

Mara ya mwisho Moscow kushika wadhifa huo ilikuwa Februari 2022, wakati wanajeshi wake walipo anzisha mashambulizi makali dhidi ya Ukraine.

CHANZO:TRT World
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us