ULIMWENGU
1 DK KUSOMA
Dalai Lama aomba radhi kwa  kumbusu mtoto mdomoni
Picha ya video iliyosambaa mtandaoni inamuonyesha kiongozi huyo wa Dini akimtolea ulimi wake mtoto mdogo wa kiume.
Dalai Lama aomba radhi kwa  kumbusu mtoto mdomoni
India Dalai Lama / Photo: AP
10 Aprili 2023

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi ya kiongozi huyo wa Buddha ilisema alitaka kuomba msamaha kwa mtoto huyo na familia yake kwa maudhi ambayo maneno yake huenda yakasababisha.

Katika picha hiyo ya Video ilimuonyesha kiongozi huyo wa kiroho Dalai Lama akimbusu mtoto kwenye midomo yake.

"Mtakatifu mara nyingi huwatania watu anaokutana nao si kwa nia mbaya, hufanya hivyo hata hadharani na mbele ya kamera. Anajutia tukio hilo," ofisi yake ilisema.

Haijabainika ni lini na wapi tukio hilo lilifanyika.

Dalai Lama amekuwa akiishi uhamishoni nchini India tangu kutoroka Tibet mwaka 1959, kufuatia maasi dhidi ya utawala wa China huko.

CHANZO:TRT Afrika na mashirika ya habari
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us